Jun 04, 2022 12:05 UTC
  • Wapalestina watolewa mwito wa kumiminika Msikiti wa Al Aqsa kukabiliana na njama ya wazayuni

Makundi mbalimbali ya Kipalestina yamewatolea mwito Wapalestina kukusanyika mnamo siku zijazo katika msikiti wa Al Aqsa kukabiliana na njama nyingine ya walowezi wa kizayuni.

Katika kukabiliana na miito iliyotolewa kwa walowezi wa kizayuni kushiriki kwenye hujuma nyingine ya kuuvamia msikiti wa Al Aqsa katika mkusanyiko uliopewa jina la "Sikukuu ya Majuma", makundi mbalimbali ya Kipalestina yametoa mwito wa kuwataka Wapalestina wakusanyike katika miskiti huo ambao ni kibla cha kwanza cha Waislamu.

Makundi hayo ya muqawama wa Palestina yamezichagua siku za Jumapili na Jumatatu wiki hii kwa Wapalestina kujumuika katika msikiti wa Al Aqsa.

Wapalestina wakikabiliana na walowezi wa Kizayuni

Hayo yanajiri katika hali ambayo Jumapili iliyopita makumi ya maelfu ya walowezi wa Kizayuni walishiriki katika kile kilichotajwa kuwa ni 'maandamano ya bendera' na kuuvamia msikiti wa Al Aqsa. 

Wazayuni hao walipambana na Wapalestina, ambapo Wapalestina wapatao 200 walijeruhiwa katika makabiliano hayo.../

Tags