Jun 23, 2022 03:54 UTC
  • Ripoti: Bin Salman kuwaruhusu Wazayuni kununua milki Makka na Madina

Tovuti moja imefichua kuwa mrithi wa ufalme wa Saudi Arabia, Mohammad Bin Salman, anatekeleza mpango ambao utawawezesha Wazayuni kununua milki katika miji mitakatifu ya Makka na Madina.

Tovuti ya Kimarekani ya Axios imesema, Marekani imekuwa ikifanya mazungumzo ya siri ya kupatanisha Saudi Arabia na utawala wa Kizayuni wa Israel ili kufanikisha mpango wa kisaliti wa kuanzishwa uhusiano wa kawaida baina ya Tel Aviv na Riyadh.

Kwa mujibu wa ripoti ya 'Saudi Leaks', Mohammad bin Salman, mrithi wa ufalme wa Saudi Arabia ametoa idhini kwa Wazayuni wa Israel kununua milki katika maeneo matakatifu ya Makka na Madina ili waweze kuimarisha satwa na ushawishi wao.

Ripoti hiyo imebaini kuwa, tayari Saudia inatayarisha mpango wa kuwaruhusu wasiokuwa raia wa nchi hiyo kununua nyumba au ardhi katika miji ya Makka na Madina. Kwa sasa sheria iliyopo hairuhusu raia yeyote asiye Msaudi kumiliki ardhi au nyumba katika miji ya Makka na Madina isipokuwa kwa njia ya urithi tu.

Yair Lapid

Ripoti hiyo imedokeza kuwa, sasa Bin Salman ameafiki kuwa mashirika ya utawala wa Kizayuni wa Israel na raia wa utawala huo wapewe idhini ya kununua nyumba au ardhi huko Makka na Madina lakini watumie pasi za kusafiria za Marekani na Ulaya.

Hivi karibuni Waziri wa Mambo ya Nje wa Utawala wa Kizayuni wa Israel, Yair Lapid alisema kuna jitihada za nyuma ya pazia za kuanzishwa uhusiano wa kawaida baina ya Israel na Saudi Arabia.

Tags