Jun 24, 2022 07:47 UTC
  • Uturuki kushirikiana na utawala wa Kizayuni wa Israel katika masuala ya usalama

Waziri wa mambo ya nje wa Uturuki Mevlut Cavusoglu amesema, baada ya kuongeza kiwango cha uwakilishi wa kidiplomasia, nchi yake itaanzisha ushirikiano wa kiusalama na utawala wa Kizayuni wa Israel.

Uturuki imekuwa ikidai kila mara kwamba inawaunga mkono wananchi madhulumu wa Palestina katika kukabiliana na jinai na kukaliwa kwa mabavu ardhi zao na utawala ghasibu wa Israel. 

Hata hivyo uungaji mkono huo umeonekana kuwa ni wa maneno matupu kutokana na Uturuki na utawala bandia wa Israel kuendelea kufanya mazungumzo ya siri katika nyanja zote. Mapema mwezi Machi mwaka huu, rais Isaac Herzog wa utawala wa Kizayuni alitembelea Uturuki kwa mwaliko rasmi wa rais wa nchi hiyo Recep Tayyip Erdoğan, ziara ambayo ilipingwa na kulalamikiwa na wananchi wa Uturuki.

Erdogan (kulia) na Herzog walipokutana mjini Ankara

Uturuki iliutambua utawala wa Kizayuni mwaka 1949, na kuanzia wakati huo pande hizo mbili zikaasisi uhusiano wa karibu katika nyuga za kiuchumi na kijeshi.

Kwa mujibu wa shirika la habari la ISNA, katika mkutano na waandishi wa habari aliofanya katika mji mkuu wa Uturuki, Ankara pamoja na waziri wa mambo ya nje wa Israel Yair Lapid, Cavusoglu amesema, hatua za Uturuki za kuongeza kiwango cha uwakilishi wa kidiplomasia na Tel Aviv imeanza katika ngazi ya ubalozi.

Aidha, waziri wa mambo ya nje wa Uturuki amesema, nchi yake haitaruhusu kufanyika mashambulio ya kigaidi katika ardhi yake na itashirikiana na Israel katika masuala ya kiusalama.

Kabla ya hapo, Cavusoglu alitoa mwito wa kustawishwa mashirikiano na utawala wa Kizayuni katika nyanja za nishati, biashara, uwekezaji, sayansi na teknolojia, kilimo na usalama wa chakula.../

Tags