Jun 24, 2022 13:27 UTC
  • HAMAS: Israel iache kuchimba mashimo kwenye ua wa Msikiti wa Al-Aqsa

Harakati ya Muqawama wa Kiislamu ya Palestina HAMAS imeutaka utawala haramu wa Israel uache mara moja kitendo chake cha kuendelea kuchimba mashimo na njia za chini kwa chini kuelekea katika msikiti mtatatifu wa al-Aqsa.

Taarifa ya HAMAS imesema, hatua ya Wazayuni kubomoa na kuchimba mashimo na njia mpya za chini kwa chini kuelekea katika Msikiti huo mtakatifu unatishia mustakabali wa Kibla hicho cha kwanza cha Waislamu.

HAMAS imeeleza kuwa, Wazayuni wanachimba mashimo katika eneo la Ukuta wa Buraq, magharibi mwa Msikiti wa al-Aqsa, na kwamba, mashimo hayo sasa ni tishio kubwa kwa ukuta wa magharibi wa msikiti huo mtukufu.

Taarifa ya harakati hiyo ya muqawama yenye makao yake katika Ukanda wa Gaza imeonya kuwa, utawala wa Kizayuni utabeba dhima kwa matokeo mabaya ya chokochoko zake hizo.

Askari katili wa Israel wakiwashambulia Waislamu katika Msiktii wa Aqsa

Itakumbukwa kuwa, tangu utawala dhalimu wa Israel ulipouvamia na kuanza kuukalia kwa mabavu mji mtakatifu wa Quds mwaka 1967 hadi sasa, umekuwa ukichimba mashimo ya chini ya ardhi katika mji huo hasa katika eneo lake la kale na kandokando mwa Msikiti wa Al-Aqsa, ili kuwalazimisha Wapalestina wayahame maeneo hayo na kuweza kuyadhibiti maeneo yanayozunguka msikiti huo mtakatifu.

Lengo la utawala vamizi wa Israel la kuchimba mashimo ya njia za chini ya ardhi chini ya Msikiti wa Al-Aqsa ni kufuta nembo na athari za Kiislamu na za kihistoria za taifa la Palestina.

Tags