Jun 29, 2022 07:44 UTC
  • Najib Miqati: Serikali ijayo ya Lebanon itatatua suala la mipaka na umeme

Waziri Mkuu wa Lebanon aliyechaguliwa kwa mara ya nne katika wadhifa huo na kupewa jukumu la kuunda baraza la mawaziri amesema kuwa, serikali mpya ya nchi hiyo italipatia ufumbuzi suala la kuianisha mipaka ya baharini kati ya nchi hiyo na utawala wa Kizayuni na kadhia ya umeme.

Duru za habari za Lebanon zimetangaza kuwa Najib Miqati amechaguliwa Waziri Mkuu wa Lebanon ambap Rais Michel Aoun wa nchi hiyo amempa jukumu kuunda serikali mpya ya nchi hiyo. Miqati ameeleza kuwa, serikali mpya ya Lebanon itakamilisha suala uanishaji wa mipaka ya baharini kati ya nchi hiyo na utawala wa Kizayuni, suala la mazungumzo na Mfuko wa Fedha wa Kimataifa (IMF) na khususan suala la umeme kati ya Lebanon na Misri, Jordan na Syria.  

Rais Michel Aoun wa Lebanon 

Amesema katika muda wa siku mbili atakuwa amekamilisha mashauriano na wabunge kuhusu namna ya kuunda serikali mpya ya Lebabon nakwamba: maslahi ya taifa ni muhimu kuliko jambo jingine lolote. 

Amesema kwa idhini yake Mola Muumba serikali ijayo ya Lebanon itatekeleza majukumu yake ipasavyo na kukamilisha kazi za serikali iliyotangulia khususan kuchukua hatua zinazohusiana na IMF, kushughulikia umeme na kuainisha mipaka ya baharini kati ya nchi hiyo na utawala wa Kizayuni. 

Ni mwaka mmoja sasa ambapo Lebabon inakabiliwa na mgogoro mkubwa kiuchumi na kisiasa. Ukosefu wa mafuta na kuongezeka bei ya sarafu ya dola khususan baada ya mlipuko mkubwa katika bandari ya Beirut yote hayo yamezidisha matatizo ya Lebanon. 

 

Tags