Jun 30, 2022 02:20 UTC
  • Uchunguzi wa maoni: Wapalestina wengi wanaunga mkono mapambano ya silaha dhidi ya Israel

Matokeo ya uchunguzi wa maoni uliyofanyika huko Palestina yanaonyesha ongezeko la uungaji mkono wa Wapalestina kwa mapambano ya silaha dhidi ya utawala haramu wa Israel na kuondolewa madarakani Mahmoud Abbas kama mkuu wa Mamlaka ya Ndani ya Palestina.

Kulingana na uchunguzi wa maoni iliyofanywa katika Ukingo wa Magharibi na Ukanda wa Gaza kati ya Juni 22 na 25 mwezi huuu wa Juni, asilimia 70 ya watu waliohojiwa wanaamini kwamba suluhisho la serikali mbili (ya Israel na Palestina) haliwezekani tena kutokana na kupanuka kwa ujenzi wa vitongoji vya walowezi wa Kizayuni katika ardhi iliyoghusubiwa na Palestina.

Wakijibu swali kwamba, ni ipi njia bora ya kukomesha uvamizi wa Israel na kuanzisha taifa huru la Palestina, washiriki wamegawanywa katika makundi matatu. Asilimia 50 ya waliohojiwa wamesema mapambano ya silaha ndiyo jibu, asilimia 22 wakiunga mkono mazungumzo na asilimia 21 ya washiriki wamesema kuwa wanaunga mkono upinzani wa amani wa wananchi.

Uchunguzi wa maoni kama huu uliofanywa miezi mitatu iliyopita pia ulionesha kuwa asilimia 44 ya waliohojiwa wanasema kuwa mapambano ya kutumia silaha dhidi ya Wazayuni maghasibu ndio chaguo bora, na asilimiia 25 walichagua mazungumzo kama njia bora zaidi ya kukomesha uvamizi wa Israel.

Kuhusu uchaguzi wa Palestina, asilimia 71 wanakubaliana na kuitishwa haraka uchaguzi mkuu wa wabunge na rais huko Palestina.

Matokeo ya uchunguzi huo wa maoni yameonesha kuwa, iwapo uchaguzi wa urais utafanyika, asilimia 33 ya Wapalestina watampigia kura Mahmoud Abbas na asilimia 55 watampigia mkuu wa Idara ya Siasa ya harakati ya Hamas, Ismail Haniyeh. Asilimia 75 ya washiriki wanataka kuondolewa madarakani Mahmoud Abbas.

Ismail Haniyeh

Sababu ya uungaji mkono mkubwa wa watu wa Palestina kwa harakati ya Hamas na Ismail Haniyeh ni utendaji na nafasi ya harakati hiyo katika kuitetea Quds tukufu na Msikiti wa Al-Aqsa hususan katika miezi ya hivi karibuni.

Tags