Jul 03, 2022 09:27 UTC
  • Nabih Berri: Kupuuzwa kadhia ya Quds kutakuwa na madhara makubwa

Spika wa Bunge la Lebanon ametahadharisha kuwa, kupuuzwa kadhia ya mji wa Quds (Jerusalem), unaokaliwa kwa mabavu na Israel, kutakuwa na madhara makubwa hasa kwa mataifa yote ya Kiarabu.

Berri ameyasemayo hayo katika kikao cha mashauriano ya mawaziri wa mambo ya nje wa Jumuiya ya Nchi za Kiarabu ambacho kimefanyika mjini Beirut kujadili hatua za pamoja za nchi wanachama wa umoja huo kuhusu Palestina.

Kwa mujibu wa Televisheni ya Al Alam, Nabih Berri, Spika wa Bunge la Lebanon amesiistiza kuhusu ulazima wa ushirikiano wa nchi zote za Kiarabu katika kutetea ukombozi wa ardhi za Palestina zinazokaliwa kwa mabavu na utawala wa Kizayuni wa Israel na kuongeza kuwa: "Tunapaswa kuwa macho kuhusu njama dhidi ya Quds na tusisalimu amri mbele ya matukio yanayojiri. Hatupaswi kusahau kuhusu kibla cha kwanza cha Waislamu."

Hali kadhalika ameashiria uwezo wa Lebanon na kusema: "Lebanon ina utajiri wa gesi na mafuta na inakaribisha uwekezaji katika sekta hii na pia katika sketa ya umeme na vituo vya usafishaji mafuta."

Mji wa Quds

Spika wa Bunge la Lebanon amesema nchi zote za Kiarabu zinapaswa kufahamu kuwa bila Palestina Waarabu hawatakuwa na utambulisho na Uarabu utaangamia iwapo Palestina itaangamia.

Naye Rais Michel Aoun  wa Lebanon amesema nchi yake haiwezi kustahamili tena idadi kubwa ya wakimbizi nchini humo na hivyo ameelezea matumaini kuwa nchi za Kiarbau zitaisaidia Lebanon katika kadhia hii ya wakimbizi.