Jul 31, 2022 11:40 UTC
  • Tawi la kijeshi la HAMAS lawaonyesha askari wawili wa Israel linaowashikilia mateka

Brigedi za Izzuddinul-Qassam, tawi la kijeshi la Harakati ya Muqawama wa Kiislamu ya Palestina, HAMAS zimetoa taswira, sambamba na kuwahutubu Wazayuni kwamba: viongozi wa utawala wa Kizayuni wanakuambieni uongo kuhusu mateka.

Julai 2014, Brigedi za Izzuddinl-Qassam zilitangaza kuwa zimemkamata mateka Shaul Aron askari wa Kizayuni katika vita vya siku 51; na utawala wa Kizayuni ukatangaza Agosti 15, 2015 kwamba umepoteza mawasiliano na askari wake Hadar Goldin huko Rafah kusini mwa Ukanda wa Gaza.

Tovuti ya habari ya Shahab News imeripoti kuwa, Brigedi za Izzuddinul-Qassam, tawi la kijeshi la Harakati ya Muqawama wa Kiislamu ya Palestina, HAMAS leo zimesambaza video inayowaonyesha Hadar Goldin na Shaul Aron, askari wawili wa Kizayuni wanaoshikiliwa mateka katika Ukanda wa Gaza.

Wapiganaji wa Brigedi za Izzuddinul-Qassam

Brigedi za al Qassam zimetangaza kuwa zimetoa video hiyo kwa anuani "utawala unakuambieni uongo" kuihutubu jamii ya Kizayuni, ili kuonyesha kuwa viongozi wa utawala haramu wa Kizayuni wa Israel wanasema uongo na wanaidanganya jamii wa Kizayuni kuhusu faili la askari wake wanaoshikiliwa mateka katika Ukanda wa Gaza.

Inafaa kuashiria kuwa, hivi sasa harakati ya Hamas inawashikilia askari wanne wa Kizayuni katika Ukanda wa Gaza ambao iliwakamata mateka katika vita vya karibuni au katika uvamizi uliofanywa na utawala haramu Israel dhidi ya Ukanda wa Gaza.../

 

Tags