Aug 04, 2022 02:34 UTC
  • Wazayuni wavamia msikiti wa al Aqsa na kuwatia nguvuni Wapalestina 12

Jeshi la utawala haramu wa Israel limewatia nguvu Wapalestina 12 sambamba na kundi la walowezi wa Kizayuni kuuhujumu msikiti mtukufu wa al Aqsa, ambacho ni Kibla cha Kwanza cha Waislamu.

Msikiti wa al Aqsa ambao ni nembo kuu ya utambulisho  wa Kiislamu-Kipalestina katika mji wa Baitul Muqaddas umekuwa ukilengwa na hujuma na hatua za uharibifu za utawala wa Israel unaoikalia Quds Tukufu kwa mabavu. 

Shirika la habari la Shihab limeripoti kuwa, kundi moja la walowezi wa Kizayuni jana liliingia kinyume cha sheria katika Msikiti wa al Aqsa na kuuvunjia heshima msikiti huo mtukufu. Wanajeshi wa Kizayuni kama kawaida wamekuwa wakiwahami na kuwaunga walowezi hao wa Kizayuni na hivyo kuwawezesha kutekeleza marasimu yao.

Msemaji wa jeshi la utawala wa Kizayuni jana Jumatano alieleza kuwa, wanajeshi wa utawala huo katika uvamizi waliofanya siku ya Jumanne na jana asubuhi wamewatia mbaroni Wapalestina 12 katika maeneo mbalimbali ya Ukingo wa Magharibi wa Mto Jordan.  

Wakati huo huo vijana wa Kipalestina jana Jumatano walikabiliana na wavamizi na maghasibu hao wa Kizayuni  katika kitongoji cha Qabatiya kusini mwa mji wa Jenin. 

Tags