Aug 12, 2022 02:24 UTC
  • Athari za mashambulio ya Yemen zinaendelea, Wakuwait wakatazwa kutumia drone Imarati

Athari za mashambulio ya kulipiza kisasi na ya kujihami ya wananchi wa Yemen dhidi ya Umoja wa Falme za Kiarabu (Imarati) bado zingalipo na sasa serikali ya Kuwait imewataka wananchi wake wasitumie ndege yoyote isiyo na rubani wanapokuwa nchini Imarati, ili wasije wakajiingiza kwenye matatizo.

Baada ya Umoja wa Falme za Kiarabu kufanya jinai kubwa dhidi ya wananchi wa Yemen kwa kushirikiana na Saudi Arabia, jeshi la Yemen liliamua kulipiza kisasi kwa kufanya mashambulizi ndani ya ardhi za Imarati na Saudia. 

Wananchi wa Yemen walitumia makombora na ndege zisizo na rubani katika mashambulio yao dhidi ya wavamizi wa nchi yao, Saudi Arabia na Umoja wa Falme za Kiarabu. Kufuatia mashambulizi hayo ya Wayemen, Wizara ya Mambo ya Ndani ya Imarati tangu wakati huo mpaka hivi sasa imepiga matufuku aina yoyote ile ya ndege isiyo na rubani kuruka nchini humo.

Moja ya ndege isiyo na rubani ya Yemen iliyotumika kushambulia Imarati kujibu mashambulio yake dhidi ya wananchi wa Yemen

 

Ubalozi wa Kuwait nchini Imarati umetoa tamko rasmi la kuwataka raia wa nchi hiyo kuheshimu sheria za Umoja wa Falme za Kiarabu kama ambavyo pia umewataka wafuate miongozo ya asasi husika wakati wowote wanapoona kuna ulazima wa kutumia drone yoyote ile wanapokuwepo Imarati.

Kabla ya kuanzisha mashambulizi ya kulipiza kisasi, Mohammad al Bukheiti, kiongozi mwandamizi wa ofisi ya kisiasa ya harakati ya Ansarullah ya Yemen alisema kuwa, nchi mbili za Saudia na Imarati zimefikia makubaliano maalumu ya kugawana ardhi ya Yemen. Saudia imekubali mikoa yote ya kusini mwa Yemen ukiwemo wa Shabwa yadhibitiwe na Umoja wa Falme za Kiarabu na kwa upande wake Imarati ilikubali kutumia nguvu zake zote za kijeshi kufanya mashambulizi dhidi ya wananchi wa Yemen.

Tags