Aug 19, 2022 08:11 UTC
  • Oman yasisitizia msimamo wake wa kutoruhusu ndege za Israel kutumia anga yake

Oman imesisitizia msimamo wake wa kukataa kuruhusu ndege za utawala wa haramu wa Israel kuruka katika anga yake.

Wakati Oman ikiendelea kusisitizia msimamo wake huo, gazeti moja ya Kiebrania limedai kwamba, eti mashinikizo ya Iran ndiyo yanayoufanya utawala wa Oman kung'ang'ania msimamo huo.

Gazeti la Israel Hayom lilidai katika chapisho lake jana kwamba, msimamo huo wa Oman ni kutekeleza takwa la Iran.

Inaelezwa kuwa, safari za ndege kupitia anga ya Oman zinaweza kutoa njia fupi za anga kwa ndege za Israel hadi Mashariki ya Mbali.

Ripoti mbalimbali ziinaeleza kuwa, "Idhini ya Oman ni muhimu sana na muhimu kwa Israeli kwa sababu, bila ridhaa yake, ndege zinazotumia anga ya Saudi Arabia haziwezi kusafiri hadi Bahari ya Hindi na kisha kwenda maeneo mbalimbali ya Mashariki.

Waziri wa Mambo ya Nje wa Oman Badr al-Busaidi

 

Ikumbukwe kuwa, akizungumza na gazeti la Kifaransa la Le Figaro mwishoni mwa mwezi wa Mei, Waziri wa Mambo ya Nje wa Oman Badr al-Busaidi alifafanua kuwa Oman haitakuwa na uhusiano wa kawaida na wa wazi na Israel hadi suala la Palestina litatuliwe.

"Oman haitajiunga na nchi za Ghuba ya Uajemi ambazo zimetangaza kuwa na uhusiano wa kawaida na utawala ghasibu wa Israel,"alisema, na kuongeza kuwa Oman "inafadhilisha mipango inayounga mkono watu wa Palestina."

Oman imekuwa ikisisitiza mara kwa mara kwamba, haitaanzisha uhusiano wa kawaida na utawala wa Kizayuni wa Israel na imekuwa ikitoa mwito wa kutatuliwa kwa haki suala la Palestina.