Sep 17, 2022 11:56 UTC
  • Umoja wa Mataifa waeleza wasiwasi wake kuhusu hali ya Ukingo wa Magharibi

Mratibu Maalumu wa Umoja wa Mataifa kwa Ajili ya Amani Mashariki ya Kati amelezea wasiwasi wake kuhusu hali ya Ukingo wa Magharibi huko Palestina inayokaliwa kwsa mabavu.

Ili kufikia malengo yao ya kujitanua zaidi, Wazayuni wamekuwa wakifanya mashambulizi ya kila siku kwenye maeneo tofauti ya Palestina na kuwakamata, kuwajeruhi au kuwaua shahidi Wapalestina kwa madai ya uwongo. Vikosi vya wanamapambano wa Palestina vinajibu jinai za utawala wa Kizayuni kwa kutekeleza operesheni maalumu.

Mratibu Maalum wa Umoja wa Mataifa wa Amani Asia Magharibi, Tor Wennesland, ameelezea wasiwasi wake juu ya kuzorota kwa hali ya usalama katika Ukingo wa Magharibi na kusisitiza kwamba kuendelezwa kwa ghasia na machafuko hakutakuwa na mshindi.

Wennesland amesema kuwa, ghasia na utumiaji mabavu vinaendeleza mgogoro na vinapaswa kusitishwa haraka iwezekanavyo.

Ukingo wa Magharibi

Katika siku chache zilizopita ardhi za Palestina zinazokaliwa kwa mabavu zimeshuhudia kushadidi kwa harakati za mapambano dhidi ya utawala wa Kizayuni, na wachambuzi wengi wa mambo wanayaona matukio hayo kuwa ni ishara ya Intifadha ya Tatu.

Kwa sasa utawala wa Kizayuni wa Israel una wogo mkubwa wa kuvurugika hali ya mambo katika Ukingo wa Magharibi wa Mto Jordan na unafanya kila uwezalo kudhibiti hali ya eneo hilo.

Hapo awali makundi ya Muqawama ya Palestina yalitangaza kuwa mapambano ya silaha ndio chaguo pekee litakalouzuia utawala wa Kizayuni kuendelea kufanya jinai dhidi ya raia wa Palestina katika ardhi zinazokaliwa kwa mabavu.

Tags