Sep 23, 2022 07:51 UTC
  • Wazayuni 8 wajeruhiwa katika oparesheni ya kujitolea kufa shahidi ya Wapalestina mjini Ramallah

Vyombo vya habari vya Kiarabu jana usiku vilitangaza habari ya kutekelezwa oparesheni ya kufa shahidi dhidi ya wanajeshi wa utawala wa Kizayuni huko Ramallah.

Wanajeshi wa utawala wa Kizayuni kwa visingizo mbalimbali kila uchao huwauwa shahidi, kuwajeruhi na kuwatia nguvuni raia wa Palestina wasio na hatia; ambapo katika kujibu jinai hizo za Israel Wapalestina pia hutekeleza oparesheni dhidi ya Wazayuni Maghasibu.  

Jana jioni Mpalestina mmoja amewashambulia kwa kisu Wazayuni kadhaa na kuwajeruhi wanane kati yao katika eneo karibu na mji wa Ramallah. Televisheni ya al Mayadeen pia imetangaza kuwa, raia aliyetekeleza oparesheni hiyo tajwa dhidi ya Wazayuni amekufa shahidi. 

Hadi sasa hakuna taarifa iliyotolewa kuhusu hali ya Wazayuni hao wanane waliojeruhiwa kwa kisu huko Ramallah. Aidha kabla ya oparesheni hiyo ya kujitolea mhanga, duru za habari ziliarifu kuhusu kutekelezwa oparesheni nyingine dhidi ya wanajeshi wa Kizayuni kusini mwa mji wa Nablus; ambapo katika oparesheni hiyo mwanajeshi mmoja wa jeshi la Israel mmoja amejeruhiwa karibu na eneo la Hawara.  

Hali ya mambo katika ardhi za Palestina inayokaliwa kwa mabavu hasa katika Ukingo wa Magharibi wa mto Jordan katika masiku ya karibuni imechukua sura maalumu; ambapo wanamapambano wa Palestina wamekuwa wakitoa jibu kwa jina zisizohesabika za Wazayuni kwa kustafidi na njia zote wanazoweza, jambo lililoibua changamoto kwa Maghasibu wa Kizayuni.   

Wanamapambano wa Palestina 

Viongozi wa utawala wa Kizayuni wamezidi kuingiwa na wahka na kukumbwa na wasiwasi kufuatia kupamba moto mapambano ya silaha ya makundi ya muqawama ya Palestina khususan katika miji miwili ya Nablus na Jenin ambayo inatambulika kama kitovu cha mapambano katika Ukingo wa Magharibi wa Mto Jordan. Hii ni kwa sababu, awali viongozi hao wa Kizayuni walikuwa wakihofa tu muqawama wa Wapalestina huko Ghaza yaani upande wa kusini lakini hivi sasa mapambano katika Ukingo wa Magharibi yamekuwa changamoto kubwa kwa watawala wa Israel; ambapo hali ya kisiasa inayolegalega sasa inashuhudiwa huko katika ardhi za Palestina zinazokaliwa kwa mabavu.  

Tags