Sep 25, 2022 02:43 UTC
  • Sheikh Naim Qassim: Iran iliwasaidia wananchi wa Lebanon, lakini Marekani inawaadhibu

Naibu Katibu Mku wa Harakati ya Mapambano ya Kiislamu ya Hizbullah ya Lebanon amesema kuwa, Iran ilikuwa pamoja na wananchi wa Lebanon katika matatizo na masaibu na iliwasaidia, lakini Marekani inawaadhibu.

Sheikh Naim Qassim ameashiria hasama na uadui wa Marekani kwa taifa la Lebanon na kusisitiza kwamba, katika hali ambayo Jamhuri ya Kiislamu ya Iran iliharakisha kuwasaidia wananchi wa Lebanon, serikali ya Marekani imeendelea kuwazingira na kutesa wananchi wa nchi hiyo.

Naibu Katibu Mku wa Harakati ya Mapambano ya Kiislamu ya Hizbullah ya Lebanon amebainisha kuwa, Iran itatekeleza ahadi yake ya kutuma tani laki 6 za nishati ya mafuta huko Lebanoni na kilichobakia hivi sasa ni kutekelezwa tu baadhi ya mambo na serikali ya Beirut ili ahadi hiyo ifanyiwe kazi.

Wananchi wa Lebanon wakishangilia na kuyakaribisha kwa kuyamwagia maua magari yaliyobeba nishati ya mafuta ya Iran

 

Kiongozi huyo mwanadamizi wa Hizbullah ya Lebanon ameishambulia Marekani kutokana na kutoheshimu ahadi zake na kueleza kwamba, lengo la Washington nii kutoa huduma kwa utawala haramu wa Israel na ndio maana imeendelea kufanya mzingiro dhidi ya Lebanon.

Naibu Katibu Mkuu wa Harakati ya Mapambano ya Kiislamu ya Hizbullah ya Lebanon amesisitiza kuwa, wananchi wa nchi hiyo katu hawatasilimu amri mbele ya matakwa haramu ya Marekani.

Kadhalika Samahat Sheikh Naim Qassim  amesema kuwa, wanaoifuata serikali ya Marekani wanapaswa kufahamu kwamba, inachokifiria Washington siku zote ni maslahi yake na maslahi ya utawala haramu wa Israel na si vinginevyo.

Tags