Sep 27, 2022 04:34 UTC
  • Al Shimi: Nembo ya muqawama wa Wapalestina katika msikiti wa al Aqsa

Wanajeshi ghasibu wa utawala wa Kizayuni wamemshambulia na kumvamia Abubakar al Shimi mzee mwenyeji wa mji wa Quds unaokaliwa kwa mabavu aliye na umri wa miaka 65 ambaye alikuwa na lengo la kuingia katika Msikiti mtukufu wa al Aqsa.

Wanajeshi wa Israel kila uchao huwashambulia raia wa Palestina, kuwauwa shahidi, kuwajeruhi na kuwatia nguvuni kwa visingizio mbalimbali. Watu walioshuhudia wameeleza kuwa, wanajeshi wa Kizayuni walimpiga mzee Abubakar al Shimi na kumburuta chini. 

Al Shimi amemweleza ripota wa Iran Press akiwa katika kituo cha matibabu alikolazwa huko Quds kwamba na hapa ninamnukuu:" Tuko tayari kujitolea maisha na watoto katika njia ya Msikiti wa Al-Aqsa." 

Mzee Abubakar al Shimi kwa miaka kadhaa sasa amekuwa akitembea kuelekea msikiti wa al Aqsa akitokea katika eneo la Ika katika ardhi za Palestina zinazokaliwa kwa mabavu.   

Hii si mara ya kwanza kwa mzee huyo Mpalestina kulengwa na mashambulizi ya Wazayuni maghasibu, hata hivyo mashambulizi hayo hayakumzuia kwenda katika msikiti wa al Aqsa; na kila mara anapoelekea huko huwa na ari zaidi. 

Walowezi vamizi wa Kizayuni kwa mara nyingine tena jana Jumatatu waliuvamia msikiti wa al Aqsa na kukabiliwa na shaari na muqawama wa Wapalestina katika eneo hilo la msikiti.  

Walowezi wa Kizayuni katika Msikiti wa al Aqsa 

Wanajeshi wa Kizayuni waliwatia nguvuni raia kadhaa wa Palestina sambamba na Wazayuni kuuvamia msikiti wa al Aqsa na wakati huo huo wanajeshi hao waliwazuia waumini wa Kipalestina kuingia katika msikiti huo mtakatifu.

Tags