Sep 29, 2022 12:06 UTC
  • Israel yapuuza azimio la UN la kusitisha ujenzi wa vitongoji vya walowezi wa Kizayuni

Mjumbe wa Umoja wa Mataifa katika eneo la Mashariki ya Kati amesema Israel inaendelea kupuuza azimio la mwaka 2016 la Baraza la Usalama la UN, linaloutaka utawala huo wa Kizayuni usitishe ujenzi wa vitongoji vya walowezi wa Kiyahudi katika ardhi za Palestina zinazokaliwa kwa mabavu.

Tor Wennesland ailiambia Baraza la Usalama jana Jumatano kwamba, Israel imepuuza azimio hilo la kuendeleza mpango wa ujenzi wa nyumba 2000 katika ardhi za Wapalestina zilizoghusubiwa, katika kipindi cha miezi mitatu iliyopita.

Mwanadiplomasia huyo wa Umoja wa Mataifa amebainisha kuwa, "tunaendelea kuona hatua chache mno zikipigwa katika utekelezaji wa azimio hilo tangu lipasishwe Disemba 2016."

Akizngumza na waandishi wa habari kufuatia kauli hiyo ya Mjumbe wa Umoja wa Mataifa katika eneo la Mashariki ya Kati, Balozi wa Palestina katika umoja huo, Riyad Mansour amelitaka baraza hilo kuchukua hatua za kivitendo kutekeleza maazimio yake.

Utawala huo ulizikaliwa kwa mabavu ardhi za Palestina katika vita vya mwaka 1967;  na azimio la Geneva linasema kuwa ni marufuku utawala wa Kizayuni kufanya shughuli zozote za ujenzi katika ardhi hizo zinazokaliwa kwa mabavu. 

Ujenzi wa vitongoji vya walowezi wa Kizayuni

Hayo yanaripotiwa katika hali ambayo, hadi sasa utawala wa Israel haujachukua hatua yoyote ya kutekeleza azimio nambari 2234 la tarehe 23 Disemba 2016 la Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa linalotaka kusitishwa ujenzi wa vitongoji vya walowezi wa Kizayuni huko Palestina inayokaliwa kwa mabavu. 

Mwezi Julai mwaka huu, Umoja wa Mataifa kwa mara nyingine tena ulipitisha azimio linalosisitiza kuwa utawala haramu wa Kizayuni wa Israel hauna haki ya kupora rasilimali za watu wa Palestina na za miinuko ya Golan ya Syria unayoikalia kwa mabavu.

Tags