Sep 30, 2022 01:23 UTC
  • Bunge la Lebanon lashindwa kumpata rais wa kumrithi Michel Aoun anayemaliza muda wake

Bunge la Lebanon jana Alkhamisi lilishindwa kumpata Rais mpya wa nchi hiyo atakayemrithi Rais Michel Aoun ambaye muhula wake wa uongozi unamalizika Septemba 31.

Bunge la Lebanon limeshindwa kumpata Rais baada ya wagombea wa kiti hicho kushindwa kupata theluthi mbili ya kura 128 za Wabunge zinazotakiwa ili atangazwe mshindi katika duru ya kwanza. Jumla ya Wabunge 122 walihudhuria kikao hicho cha Bunge kilicholenga kumchagua Rais huuu Wabunge 63 kati yao wakirejesha karatasi za kura zikiwa nyeupe pasi na kumchagua mgombea yoyote kati ya waliojitokeza.

Michel Moawad alishika nafasi ya kwanza katika kinyang'anyiro hicho akipata kura 36  kati ya 122 za Wabunge waliohudhuria kikao hicho.

Makundi ya kisiasa Lebanon yanaamini kuwa, kuchaguliwa rais na kupatikana serikali kutapelekea mchakato wa kisiasa nchini humo kuingia awamu mpya huku nguvu zikielekezwa katika utatuzi wa matizo yaliyopo hivi sasa hasa ya kiuchumi.

Michel Aoun Rais wa Lebanon anayemaliza muda wake wa uongozi

 

Lebanon imekuwa ikikabiliwa na maandamano makubwa tangu Oktoba 2019 kupinga hali mbaya ya maisha, mfumo wa bei na kudorora uchumi wa maandamano ambayo yalipelekea kujiuzulu kwa Waziri Mkuu Saad al-Hariri na baada ya hapo nchi hiyo ikatuumbukia katika mzozo na mvutano mkubwa kisiasa.

Katika kipindi ambacho Lebanon haijawa na serikali imekumbwa na matatizo mengi yakiwemo maandamano, kudhoofika uchumi na changamoto za usalama. Aidha utawala wa Kizayuni wa Israel umekuwa ukitumia vibaya ombwe la kuutokuweko serikali imara nchini Lebanmon kwa ajili ya kuongeza chokochojko zake katika mipaka ya kusini mwa Lebanon na hivyo kuhatarisha kujitawala kwa nchi hiyo ya Kiarabu.