Oct 07, 2022 02:36 UTC
  • Kukiri Waziri Mkuu wa UK kwamba yeye ni Zayuni

Liz Truss ambaye ni karibu mwezi mmoja tu nyuma ameanza kazi ya uwaziri mkuu wa Uingereza, amejitokeza hadharani na kutangaza kuwa yeye ni Zayuni "la kutupwa" yaani Mzayuni mkubwa sana na amesema atahakikisha uhusiano wa London na Wazayuni utaimarika mno wakati wa uongozi wake.

Waziri mkuu huyo wa Uingereza ametangaza uungaji wake mkono kwa Wazayuni kiasi chote hicho wakati ambapo hakuna chochote kipya kwa nchi za Magharibi kwani kwa miaka mingi nchi hizo hasa Uingereza na Marekani ni waungaji mkubwa mno wa jinai za utawala wa Kizayuni tena kwa kila upande.

Kwa makumi ya miaka sasa utawala wa Kizayuni unawafanyia dhulma na jinai kubwa Wapalestina, unawaua kikatili na unaendelea kuwapora ardhi zao na sehemu yake kujenga vitongoji vya walowezi wa Kizayuni huku jamii ya kimataifa ikiendelea kukaa kimya bila ya kuchukua hatua za kuilazimisha Israel ikomeshe jinai zake hizo. Si hayo tu, lakini pia madola ya kibeberu kama Marekani na Uingereza yanazuia hata kuwafikia Wapalestinna misaada ya madawa na matibabu, yote ikiwa ni kwa shabaha ya kuusaidia utawala wa Kizayuni uendeleze ukatili wake dhidi ya Wapalestina. Siasa hizo zinawakasirisha watu wengi duniani na sasa kila mwenye mtazamo huru anakubali kuwa Wapalestina wanadhulumiwa. Lakini kama tulivyosema, viongozi wa nchi za Magharibi hasa Uingereza na Marekani wanatangaza waziwazi kuunga mkono jinai hizo za Israel na hivi sasa tunamuona waziri mkuu wa Uingereza akisema mbele ya kadamnasi ya watu kuwa yeye ni Mzayuni mkubwa sana na atahakikisha uhusiano wa nchi yake na Wazayuni unakuwa mkubwa zaidi wakati wa uongozi wake. Mtu unajiuliza, Liz Truss anataka kuongeza nini kipya katika uhusiano huo wakati hakuna sehemu iliyobakia tupu? Au ameamua kujikomba tu kwa Wazayuni wenzake?

Sami Abu Zuhri

 

Sami Abu Zuhri, mmoja wa viongozi wa ngazi za juu wa Harakati ya Mapambano ya Kiislamu ya Palestina HAMAS anasema: Matamshi ya Liz Truss ya kuunga mkono utawala wa Kizayuni maana yake ni kutangaza kuwa yuko pamoja na jinai zinazofanywa na utawala wa Kizayuni dhidi ya wananchi wa Palestina. Ni watu wa namna hii ndio wanaochochea kuendelea kuuliwa watoto wadogo wasio na hatia na wanasimama imara kuficha jinai hizo.

Katika upande mwingine, kitendo cha nchi za Magharibi cha kuipa Israel kiwango kikubwa cha silaha za kufanyia jinai na ukatili, ni miongoni mwa mambo yanayolalamikiwa mno na makundi ya kutetea haki za Wapalestina. Hivi karribuni kundi moja la watetezi wa Palestina lilikusanyika mbele ya benki ya Berkley mjini Manchester huko Uingereza na kuitaka nchi hiyo iache kutumia fedha za wananchi kuupa silaha utawala wa Kizayuni. Taasisi hiyo ya kupiga vita umaskini imesema, uongozi wa benki ya Berkley ndio unaogharamia fedha za silaha za utawala wa Kizayuni na kuchochea jinai na mauaji ya Wazayuni dhidi ya wananchi wasio na ulinzi wa Palestina.

Liz Truss, waziri mkuu wa Uingereza aliyejigamba kuwa yeye ni "Zayuni la kutupwa"

 

 

Abdel-Latif al-Qanou ni msemaji wa Harakati ya Mapambano ya Kiislamu ya Palestina HAMAS. Yeye anasema, uamuzi wa Liz Truss wa kuhamishia Quds ubalozi wa Uingereza kutoka Tel-Aviv na kutangaza waziwazi uungaji mkono wake kwa utawala wa Kizayuni, ni kutangaza rasmi uadui wa Uingereza kwa taifa la Palestina. Ameongeza kuwa, mji wa Baytul Muqaddas ni ardhi ya Palestina inayokaliwa kwa mabavu na Wazayuni. Mji huu ni mali ya taifa letu. Kuhamishia Quds ubalozi wowote ule hakuwezi kubadilisha uhakika huo wa kihistoria.

Ukweli ni kuwa Wapalestinna hawana matumaini hata chembe ya kuungwa mkono na madola ya Magharibi. Matumaini yao wameyaelekeza kwenye uungaji mkono wa mamilioni ya watu wenye fikra huru katika pembe mbalimbali za dunia ambao mara kwa mara wamekuwa wakichukua hatua za kuonesha uungaji mkono wao kwa malengo matukufu ya ukombozi wa Palestina. Aidha inaonekana wazi kabisa kwamba Wapalestina hawakushangazwa na hatua ya waziri mkuu wa Uingereza, Lizz Truss ya kutoka hadharani na kuutangazia ulimwengu kuwa yeye ni Mzayuni mkubwa.

Tags