-
Baraza la Usalama laendelea kufumbia macho mapigano Tigray, Ethiopia
Mar 06, 2021 08:15Jitihada za kulitaka Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa litoe taarifa ya kutaka kusitishwa machafuko na mauaji yanayoendelea kushuhudiwa katika eneo la Tigray, kaskazini mwa Ethiopia zimegonga mwamba.
-
UN: Majeshi ya Eritrea, Ethiopia yumkini yamefanya jinai za kivita Tigray
Mar 05, 2021 02:32Kamishna wa Haki za Binadamu wa Umoja wa Mataifa amesema ofisi yake ina ithibati ya kufanyika jinai za kutisha ambazo zinaweza kuwa jinai za kivita na jinai dhidi ya binadamu zilizofanywa na wanajeshi wa Ethiopia na Eritrea katika eneo la Tigray.
-
Ethiopia yataka kutatuliwa hitilafu za mpaka na Sudan kwa njia za amani
Mar 04, 2021 04:15Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nchi za Nje ya Ethiopia amesema kuwa, Addis Ababa inataka kutatua hitilafu zake za mpaka na Sudan kwa njia za amani na haitaingia vitani kutokana na kadhia hiyo.
-
Wafanyakazi wanne wa sekta ya habari watiwa mbaroni katika eneo la Tigray, Ethiopia
Mar 02, 2021 10:50Wafanyakazi wanne wa sekta ya habari katika eneo lililoathiriwa na machafuko la Tigray nchini Ethiopia wametiwa mbaroni na kushikiliwa korokoroni. Hayo yameelezwa na familia na wafanyakazi wenzao.
-
Amnesty: Jeshi la Eritrea liliua mamia ya raia Ethiopia Novemba 2020
Feb 26, 2021 08:03Shirika la kutetea haki za binadamu la Amesty International limesema mauaji ya kiholela ya mamia ya raia yaliyofanywa na jeshi la Eritrea katika mji wa kale wa Ethiopia wa Axum Novemba mwaka jana ni ukiukaji wa wazi wa haki za binadamu na ukanyagaji wa sheria za kimataifa za kumlinda mwanadamu.
-
Sudan yataka upatanishi wa kimataifa kuhusu mgogogoro wa Bwawa la al-Nahdha
Feb 24, 2021 02:42Waziri wa Umwagiliaji na Vyanzo vya Maji wa Sudan amesema kuwa, nchi yake inakusudia kuandaa uungaji mkono na upatanishi wa pande nne kwa ajili ya kupatiwa ufumbuzi mzozo wa Bwawa la al-Nahdha.
-
Umoja wa Afrika waanza upatanishi katika mzozo wa Sudan na Ethiopia
Feb 18, 2021 11:00Duru za kuaminika nchini Sudan zimeripoti kuwa, mjumbe wa Umoja wa Afrika alitazamiwa kuwasili Khartoum akiongoza ujumbe wa upatanishi wa umoja huo katika mzozo wa mpakani baina ya Sudan na Ethiopia.
-
Ethiopia yakubali kwa masharti upatanishi baina yake na Sudan
Feb 15, 2021 01:24Serikali ya Ethiopia imetangaza kuwa imekubali upatanishi wa nchi nyingine katika mgogoro baina yake na nchi jirani ya Sudan lakini kwa masharti.
-
UN yataka mashirika ya misaada yapewe uhuru wa kuingia Tigray, Ethiopia
Feb 14, 2021 03:45Msemaji wa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa ameitaka serikali ya Ethiopia iruhusu mashirika ya misaada kuingia na kufanya kazi zake kwa uhuru katika eneo la Tigray ili kuokoa roho za wakazi wa eneo hilo.
-
UNICEF: Watoto wanateseka katike eneo lenye mgogoro la Tigray, Ethiopia
Feb 13, 2021 04:50Kadri misaada ya dharura na wafanyakazi wa kusambaza misaada hiyo wanafikia eneo la mzozo la Tigray huko Ethiopia, taswira halisi ya masikitiko inazidi kuibuka jinsi watoto kwenye eneo hilo wanavyoendelea kuteseka.