-
Zarif: Iran iko tayari kushirikiana na Russia kuhusu maeneo ya Caucasia na Ghuba ya Uajemi
Jan 27, 2021 04:27Waziri wa Mambo ya Nje wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran amesema ushirikiano wa Iran na Russia ni kwa ajili ya amani na uthabiti katika eneo. Ameongeza kuwa: "Tuko tayari kushirkiana na Russia katika masuala ya Caucasia na Ghuba ya Uajemi."
-
Amir Abdolahian: Uhusiano wa Iran, China na Russia ni wa kiistratijia
Jan 26, 2021 11:10Mshauri Mkuu wa wa Spika wa Majlisi ya Ushauri ya Kiislamu (bunge la Iran) katika masuala ya kimataifa amesema kuwa, uhusiano wa Tehran, Beijing na Moscow ni wa kiistratijia na kuongeza kuwa, uhusiano na nchi za dunia ambazo zilikuwa pamoja na wananchi wa Iran wakati wa hali ngumu umejengeka juu ya msingi na stratijia ya urafiki, ushirikiano na kuheshimiana.
-
Balozi wa Iran UN: Rais wa Marekani achukue hatua ya kwanza
Jan 26, 2021 07:35Balozi na Mwakilishi wa Kudumu wa Iran katika Umoja wa Mataifa amesema Jamhuri ya Kiislamu haina mpango wowote wa kufanya mazungumzo na Rais mpya wa Marekani Joe Biden, lakini inasubiri serikali mpya ya Washington ichukue hatua ya kwanza ya kuliondolea taifa hili vikwazo na kurejea katika makubaliano ya nyuklia ya JCPOA.
-
Dozi zaidi ya milioni 16 za chanjo ya corona kuingizwa nchini Iran hivi karibuni
Jan 25, 2021 12:46Mkuu wa kamati ya afya na tiba ya Majlisi ya Ushauri ya Kiislamu ya Iran amesema, taratibu zinakamilishwa kwa ajili ya kuingiza nchini dozi 16,800,000 za chanjo ya corona kutoka nchi zenye kuaminika na zilizokubalika.
-
Polisi Sudan wakabiliana na waandamanaji wanaolalamikia ughali wa maisha
Jan 25, 2021 07:39Polisi nchini Sudan wamelazimika kutumia gesi ya kutoa machozi kuwatawanya waandamanaji waliokuwa na hasira katika mji mkuu Khartoum ambao walikuwa wanalalamikia ugali wa maisha.
-
Wapalestina: Iran ndiye muungaji mkono mkuu wa ukombozi wa Palestina
Jan 25, 2021 02:31Harakati ya Jihadul Islami ya Palestina imesema kuwa, Jamhuri ya Kiislamu ya Iran ndiye muungaji mkono mkuu wa ukombozi wa Palestina na muqawama wa taifa hilo mbele ya jinai za utawala wa Kizayuni.
-
Waziri wa Afya wa Iran: Utoaji chanjo ya corona nchini utaanza hivi karibuni
Jan 24, 2021 14:01Waziri wa Afya, Tiba na Mafunzo ya Utabibu ya Iran amesema, utoaji chanjo ya corona hapa nchini utaanza hivi karibuni.
-
Rouhani: Iran kuanza kutoa chanjo ya Covid-19 ndani ya siku chache zijazo
Jan 23, 2021 12:12Rais Hassan Rouhani wa Iran amesema Jamhuri ya Kiislamu itaanza kutoa chanjo ya kukabiliana na ugonjwa wa Covid-19 hapa nchini katika kipindi cha siku chache zijazo.
-
Zarif: Mlango wa fursa kwa utawala mpya wa Marekani hautabaki wazi milele
Jan 23, 2021 11:49Waziri wa Mambo ya Nje wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran amemuasa Rais mpya wa Marekani Joe Biden, ahitimishe sera za mashinikizo zilizogonga mwamba za mtangulizi wake Donald Trump na kusisitiza kuwa, "dirisha la fursa kwa timu mpya ya Ikulu ya White House halitabakia wazi milele."
-
Iran kuanzisha kituo kikubwa zaidi cha Teknolojia nchini Kenya
Jan 23, 2021 05:06Jamhuri ya Kiislamu ya Iran imetangaza kuanzisha kituo kikubwa cha ubunifu na teknolojia katika mji mkuu wa Kenya, Nairobi ikiwa ni katika mkakati wa kuimarisha uhusiano wa nchi hizi mbili rafiki.