-
Harakati ya Nujabaa: Kuendelea kuwepo kijeshi Marekani ndio hatari kubwa zaidi kwa Iraq
Apr 15, 2021 13:02Naibu Katibu Mkuu wa harakati ya muqawama wa Kiislamu ya Nujabaa nchini Iraq amesisitiza kuwa, kuendelea kuwepo kijeshi Marekani, ndio hatari kubwa zaidi inayotishia usalama wa Iraq.
-
Msafara wa wanajeshi vamizi wa Marekani washambuliwa kusini mwa Iraq
Apr 14, 2021 02:36Duru za habari za Iraq zimetangaza kuwa, msafara wa magari yaliyokuwa yamepakia vifaa mbalimbali na zana za kijeshi kwa ajili ya wanajeshi vamizi wa Marekani umeshambuliwa kusini mwa nchi hiyo.
-
Ndege za kivita za Iraq zashambulia ngome za magaidi wa ISIS nchini Iraq
Apr 11, 2021 07:45Ndege za kivita za Iraq zimeshambulia ngome za magaidi wa ISIS au Daesh katika Milima ya Hamrin mkoani Diyala ambapo magaidi kadhaa wameangamizwa
-
Tathmini ya kikao cha tatu cha Baghdad na washington
Apr 08, 2021 02:37Duru mpya ya mazungumzo ya kistratijia baina ya Baghdad na Washington ilianza jana Jumatano kwa njia ya video. Taarifa iliyotolewa huko nyuma na Wizara ya Mambo ya Nje ya Marekani ilisema kuwa mazungumzo hayo yatahusu usalama, namna ya kupambana na ugaidi, nishati na masuala ya kisiasa.
-
Makundi ya Muqawama ya Iraq yatishia kushambulia vikosi vya majeshi ya Marekani
Apr 07, 2021 12:13Makundi ya Muqawama na mapambano ya Iraq yametishia kutoa vipigo vikali na makini kwa majeshi vamizi ya Marekani yaliyoko nchini humo iwapo Baghdad na Wshington hazitatangaza muda maalumu wa kuondoka majeshi hayo katika ardhi ya Iraq.
-
Kwa nini baadhi ya Wairaqi wamepinga safari ya al Kadhimi nchini Saudi Arabia
Apr 04, 2021 02:32Safari ya Waziri Mkuu wa Iraq, Mustafa al Kadhimi nchini Saudi Arabia imekabiliwa na upinzani wa baadhi ya shakhsia na wanasiasa ndani ya Iraq.
-
Kamati ya pamoja ya Iran na Iraq yachunguza mauaji ya kigaidi ya Soleimani
Apr 03, 2021 09:43Mkuu wa Baraza Kuu la Haki za Binadamu la Vyombo vya Mahakama vya Iran amesema faili la mauaji ya kigaidi ya Shahid Qassem Soleimani, aliyekuwa Kamanda wa Kikosi cha Quds cha Jeshi la Walinzi wa Mapinduzi ya Kiislamu la Iran (IRGC) linafuatiliwa na kamati ya pamoja ya Iran na Iraq.
-
Iraq na Syria zaendelea na mazungumzo kuhusu kurudi nyumbani wakimbizi
Apr 02, 2021 06:34Nchi mbili za Iraq na Syria zinaendelea na mazungumzo baina yao kuhusu namna ya kuwarejesha makwao wakimbizi wa nchi hizo mbili waliokimbilia katika nchi hizo.
-
Ukosoaji kufuatia kuongezeka hatua za Imarati za kujipenyeza kiintelijinsia na kisiasa huko Iraq
Mar 31, 2021 10:42Katika masiku ya karibuni suala la kujipenyeza Umoja wa Falme za Kiarabu (Imarati) huko Iraq kwa mara nyingine tena limezungumziwa pakubwa. Shakhsia na vyombo vya habari vya Iraq vimetangaza kuwa Imarati imezidisha satwa yake ya kiintelijinsia na kisiasa nchini humo.
-
Maafisa Usalama Iraq wazima jaribio la shambulizi la kigaidi Karbala
Mar 29, 2021 12:34Maafisa usalama wa Iraq wamezima jaribio la shambulizi la kigaidi lililolenga mjumuiko mkubwa wa wapenzi wa Watu wa Nyumba ya Mtume Muhammad (saw) uliokuwa njiani kutoka Najaf ukielekea katika mji mtakatifu wa Karbala kwa ajili ya sherehe za kuzaliwa Imam wa Zama na mwokozi aliyeahidiwa wa Akheri Zamani, Imam Mahdi (as).