• Kikao cha Baraza la Usalama la UN kuhusu usalama wa Ghuba ya Uajemi

  Oct 21, 2020 12:18

  Eneo la Ghuba ya Uajemi ambalo ni miongoni mwa maeneo ya kistratijia ya dunia na yenye umuhimu mkubwa katika soko la kimataifa la masuala ya uchumi na nishati. Kwa kuzingatia uhakika huo usalama wa eneo hilo muhimu la majini daima umekuwa ukipewa mazingatio makubwa katika taasisi za Umoja wa Mataifa.

 • Guterres: Mapatano ya JCPOA ni muhimu mno kwa usalama wa Ghuba ya Uajemi

  Oct 21, 2020 07:30

  Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, António Guterres amesema katika mkutano uliofanyika kwa njia ya Intaneti kwamba kulindwa na kuhifadhiwa mapatano ya kimataifa ya nyuklia yanayojulikana kwa jina maarufu la JCPOA ni muhimu mno kwa usalama wa eneo la Ghuba ya Uajemi.

 • Iran: Leo ni siku muhimu kwa walimwengu baada ya kufikia tamati vikwazo vya silaha dhidi ya Tehran

  Oct 18, 2020 08:20

  Wizara ya Mashauri ya Kigeni ya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran imetoa taarifa rasmi kwa mnasaba wa siku ya leo ya tarehe 18 Oktoba ya kufikia tamati muda wa vikwazo vya silaha dhidi ya taifa hili na kueleza kwamba, hii ni siku muhimu kwa jamii ya kimataifa.

 • Mitazamo ya Trump na Biden kuhusu Iran; madai ya ushindi mkabala na kukiri kwamba Marekani imetengwa

  Oct 18, 2020 02:28

  Katika kipindi hiki cha kukaribia uchaguzi wa Rais nchini Marekani tarehe 3 Novemba mwaka huu Rais Donald Trump wa nchi hiyo ambaye ni mgombea wa chama cha Republican na Joe Biden wa chama cha Democratic wamekuwa wakizungumzia kadhia ya Iran na mapatano ya nyuklia ya JCPOA katika kampeni zao za uchaguzi lakini kwa mitazamo tofauti na inayokinzana.

 • Ndoto za alinacha za Trump za kufanya mazungumzo na Jamhuri ya Kiislamu ya Iran

  Oct 14, 2020 02:23

  Rais Donald Trump wa Marekani akiwa na lengo la kujijengea nafasi nzuri wakati huu wa kukaribia uchaguzi nchini humo, anahitajia kutoa madai ya kufanikiwa katika sera za kigeni za nchi hiyo hasa kuhusiana na Iran.

 • Borell akiri udharura wa Iran kunufaika na mkataba wa JCPOA

  Oct 09, 2020 07:13

  Licha ya kuwa Umoja wa Ulaya na Troika ya Ulaya ambayo inajumuisha nchi za Ujerumani, Ufaransa na Uingereza zilikuwa na mchango mkubwa katika kufanikisha mapatano ya nyuklia ya Iran yanayojulikana kama JCPOA, lakini baada ya Marekani kujitoa katika mapatano hayo, pande hizo zimekuwa na utendaji mbaya usioweza kutetewa kutokana na kuwa zimeshindwa kuyalinda na pia kutotekeleza ahadi zao, na hasa kuhusu kutofanikisha mfumo wa mabadilishano ya kifedha na kibiashara unaojulikana kama Instex.

 • Kurejea kwenye mapatano ya nyuklia ya JCPOA, hatua ya kwanza inayopasa kuchukuliwa na Marekani

  Sep 27, 2020 04:08

  Rais Donald Trump wa Marekani amekuwa akiyataja mapatano ya nyuklia ya JCPOA kuwa ndiyo mapatano mabaya zaidi kwa nchi yake na hatimaye mwezi Mei mwaka 2018 aliiondoa nchi hiyo kwenye mapatano hayo na kuiwekea Jamhuri ya Kiislamu ya Iran vikwazo vikali. Hivi sasa Joe Biden mgombea wa kiti cha urais wa chama cha Democratic huko Marekani amesema iwapo atashinda uchaguzi huo wa mwezi Novemba mwaka huu atairejesha Marekani katika mapatano hayo ya JCPOA.

 • Tarehe 20 Septemba; Marekani kupata pigo jingine?

  Sep 19, 2020 04:27

  Waziri wa Mashauri ya Kigeni wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran amesema kuwa, hakuna kitu kipya kitakachotokea kesho tarehe 20 Septemba na kwamba, inamtosha kwa Waziri wa Mashauri ya Kigeni wa Marekani kulisoma azimio nambari 2231 la Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa.

 • Ombi la Guterres kwa nchi mbalimbali kufanya juhudi za pamoja ili kuyalinda mapatano ya JCPOA

  Sep 17, 2020 08:50

  Baada ya Marekani kujitoa kwa upande mmoja katika mapatano ya nyuklia ya JCPOA mwezi Mei mwaka 2018 hivi sasa nchi wanachama zilizosalia katika kundi la 4+1 zinasisitiza kuendelea kuwepo mapatano hayo kinyume na mtazamo wa Washington ambayo ilitaka kuchukuliwa hatua sawa na hiyo kutoka kwa wanachama wengine wa kundi la 5+1. Hvi sasa Marekani inafanya njama zake zote kujaribu kuyasambaratisha mapatano hayo ya JCPOA.

 • Iran: Makubaliano yoyote hayatodumu mpaka yatekeleze sawa haki na majukumu

  Sep 17, 2020 02:22

  Naibu Waziri wa Mambo ya Nje wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran katika masuala ya haki za kimataifa amesema kuwa, makubaliano yoyote yale ya kimataifa hayawezi kudumu bila ya kuweko mlingano sawa katika utekelezaji wa haki na majukumu, na kwamba mapatano ya nyuklia ya JCPOA nayo hayawezi kutoka kwenye msingi huo.