-
Umoja wa Mataifa watangaza tarehe ya uchaguzi wa Serikali ya Mpito Libya
Jan 22, 2021 11:53Ujumbe wa Umoja wa Mataifa nchini Libya umetangaza kuwa, wagombea wa nafasi za uongozi katika serikali mpya ya mpito ya Libya wanatakiwa wajulikane katika kipindi cha wiki moja ijayo ili mwanzoni mwa mwezi ujao wa Februari kupigwe kura ya kuwachagua wagombea hao.
-
Misri yakaribisha mapatano ya Libya kuhusu mchakato wa katiba ya nchi hiyo
Jan 21, 2021 11:53Wizara ya Mambo ya Nje ya Misri imekaribisha mapatano yaliyofikiwa na pande za Libya kuhusu mchakato wa katiba ya nchi hiyo.
-
UN yatoa wito wa kurejeshwa operesheni za uokozi baada ya wahajiri 43 kupoteza maisha
Jan 21, 2021 07:41Mashirika ya Umoja wa Mataifa ya uhamiaji IOM na lile la kuhudumia wakimbizi UNHCR yametoa wito kwa nchi kurejesha operesheni za kuwasaka na kuwaokoa watu kwenye bahari ya Mediterania baada ya wahajiri wengine 43 kupoteza maisha katika ajali ya boti iliyotokea siku ya Jumatatu katika pwani ya Libya.
-
Mkuu wa UN ataka askari ajinabi waondoke Libya haraka iwezekavyo
Jan 19, 2021 11:57Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa ametaka wanajeshi na mamluki wote wa nchi ajinabi waondoke nchini Libya haraka iwezekanavyo.
-
Uchaguzi wa kwanza nchini Libya mwaka huu wa 2021
Jan 09, 2021 11:22Sambamba na juhudi za kidiplomasia zinazofanyika kwa shabaha ya kupata ufumbuzi wa mgogoro wa Libya na hatimaye kufikia mapatano ya kudumu ya kisiasa, kumefanyika uchaguzi wa kwanza wa mabaraza ya miji katika nchi hiyo ya kaskazini mwa Afrika.
-
Russia: waungaji mkono wa Gaddafi wanapasa kushiriki mazungumzo ya Libya
Jan 05, 2021 02:18Naibu Waziri wa Mambo ya Nje wa Russia ameeleza kuwa waungaji mkono wa dikteta wa zamani wa Libya wanapasa kushirikishwa katika mazungumzo ya amani ya nchi hiyo.
-
Walibya wavamia makazi ya kijeshi ya Haftar, wataka kulipiza kisasi dhidi ya mamluki
Jan 01, 2021 13:25Wakazi wa mji wa Houn katika eneo la al Jufra huko katikati mwa Libya wamefanya maandamano wakitaka kulipiza kisasi kwa mamluki wa kampuni ya Wagner ya Russia na wapiganaji wa kundi la Janjaweed kutoka Sudan wanaolisaidia jeshi la jenerali muasi, Khalifa Haftar baada ya mauaji ya raia kadhaa wa eneo hilo.
-
Misri yaahidi kufungua tena ubalozi wake nchini Libya
Dec 28, 2020 08:10Serikali ya Misri imetangaza kuwa, karibuni hivi itafungua tena ubalozi wake katika nchi jirani ya Libya.
-
Uingiliaji wa kigeni nchini Libya; chanzo cha kuvunjika mazungumzo ya amani
Dec 18, 2020 02:49Uingiliaji wa nchi za nje katika masuala ya ndani ya Libya unaendelea katika hali ambayo duru mpya ya mazungumzo ya amani ya nchi hiyo imevunjika kutokana na tofauti zilizoibuka kuhusu namna ya kuwachagua wanachama wa baraza la mawaziri.
-
Baraza la Usalama lataka mamluki wote waondoke nchini Libya
Dec 17, 2020 04:37Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa limetoa mwito wa kuondoka mara moja mamluki na wapiganaji wote wa nchi ajinabi nchini Libya.