-
Viongozi wa Sudan wapiga marufuku maandamano ya aina yoyote
Apr 30, 2022 11:25Viongozi wa Sudan wametangaza kupiga marufuku maandamano yoyote yale kwa mnasaba wa miaka mitatu ya maandamano ya kulalamikia madaraka ya nchi kutwaliwa na wanajeshi wa nchi hiyo.
-
Watetezi wa Palestina wafanya maandamano mbele ya ubalozi wa Israel mjini New York
Apr 22, 2022 01:52Makundi ya wapinzani wa utawala ghasibu wa Israel yamefanya maandamano mbele ya ubalozi mdogo wa Tel Aviv mjini New York, Marekani na kutangaza uungaji mkono wao kwa wananchi madhulumu wa Palestina. Maandamano hayo yamefanyika kupinga ukatili na jinai zinazoendelea kufanywa na utawala wa Kizayuni wa Israel huko katika ardhi zinazokaliwa kwa mabavu za Palestina.
-
Wamorocco, Wabahrain, Waturuki waandamana kuitetea Aqsa, Syria, Kuwait zatoa kauli
Apr 17, 2022 08:17Wananchi wa Morocco wamefanya maandamano makubwa katika mji mkuu wa nchi hiyo, Rabat kutangaza uungaji mkono wao kwa wananchi wa Palestina, sanjari na kulaani kitendo cha utawala haramu wa Israel cha kuuvamia na kuuvunjia heshima Msikiti wa al-Aqsa.
-
Wanigeria waandamana kutaka Zakzaky apewe paspoti yake
Apr 12, 2022 10:27Wananchi wa Nigeria wamefanya maandamano katika mji mkuu wa nchi hiyo Abuja, kuishinikiza serikali ya nchi hiyo impe Sheikh Ibrahim Zakzaky, Kiongozi wa Harakati ya Kiislamu ya nchi hiyo pasipoti yake ya kusafiria iliyotwaa.
-
Macron na Le Pen waingia duru ya pili uchaguzi wa rais Ufaransa, ushiriki umepungua
Apr 11, 2022 11:50Rais anayemaliza muda wake wa Ufaransa, Emmanuel Macron na mgombea mwenye siasa kali za mrengo wa kulia wa , Marine Le Pen wameongoza matokeo ya duru ya kwanza ya uchaguzi wa rais wa Ufaransa uliofanyika jana Jumapili, na wakahamia duru ya pili kati ya hizi. uchaguzi uliopangwa kufanyika Aprili 24.
-
Wayemen wafanya maandamano ya kulaani uvamizi na vita dhidi ya nchi yao
Mar 27, 2022 02:31Wananchi wa Yemen katika mkoa wa Saada jana Jumamosi walimiminika mabarabarani kushiriki maandamano ya kupinga na kulaani moto wa vita uliowashwa na Saudi Arabia na washirika wake dhidi ya nchi hiyo maskini kuanzia mwezi Machi 2015 na kuendelea hadi sasa.
-
Maandamano ya Wasudani milioni moja kufanyika leo, wanapinga utawala wa kijeshi
Mar 21, 2022 07:47Makundi yanayopinga utawala wa kijeshi nchini Sudan yameitisha maandamano ya watu milioni moja leo Jumatatu, ambayo wamesema yataelekea katika ikulu ya rais katikati mwa mji mkuu, Khartoum. Maandamano ya leo ya Wasudani yanafuatia yale yaliyofanyika usiku wa kuamkia leo katika miji mingine kadhaa ya Sudan.
-
Waturuki wabeba picha za Shahidi Soleimani wakiandamana dhidi ya Israel
Mar 12, 2022 13:24Wananchi wa Uturuki jana Ijumaa, kwa mara nyingine tena walimiminika mabarabarani katika maandamano ya kulaani ziara tata ya rais wa utawala wa Kizayuni wa Israel nchini mwao.
-
Wasudan waandamana tena kupinga utawala wa kijeshi, 50 wajeruhiwa
Mar 04, 2022 12:17Zaidi ya watu 50 wamejeruhiwa katika maandamano ya kupinga utawala wa kijeshi katika mji mkuu wa Sudan, Khartoum na miji mingine mikubwa ya nchi hiyo.
-
Walebanoni waandamana kuunga mkono operesheni ya kijeshi ya Russia nchini Ukraine
Mar 04, 2022 08:04Wakazi wa mji mkuu wa Lebanon, Beirut wamefanya maandamano wakishirikiana na Warussia wanaoishi nchini humo wakiunga mkono operesheni ya Jeshi la Russia dhidi ya "mafashisti wa Ukraine".