-
Zakharova: Marekani inawatambua washindani wake wakuu kuwa ni maadui
Mar 05, 2021 07:48Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nchi za Nje ya Russia amesema kuwa nchi yoyote inayoshindana na Marekani katika uwanja wowote ule hutambuliwa na Washington kuwa ni nchi adui.
-
Kuanza kampeni kubwa ya vikwazo ya serikali ya Biden dhidi ya Russia
Mar 05, 2021 02:29Uhusiano wa Marekani na Russia katika serikali mpya ya Marekani na wakati huu wa uongozi wa Joe Biden umezidi kuwa mbaya. Serikali ya Biden mbali na kudhihirisha misimamo iliyodhidi ya Russia, hivi sasa imeanzisha kampeni kubwa ya vikwazo dhidi ya Moscow.
-
Russia: Mashambulio ya Marekani Syria ni ukiukaji wa kanuni na sheria za kimataifa
Feb 26, 2021 13:14Wizara ya Mambo ya Nje ya Russia imelaani mashambulizi ya usiku wa kuamikia leo ya Marekani huko Syria na kuyataja kuwa ni kinyume na kanuni na sheria za kimataifa.
-
Safari ya Waziri wa Mambo ya Nje wa Afghanistan nchini Russia
Feb 26, 2021 02:53Waziri wa Mambo ya Nje wa Afghanistan ameelekea Moscow, mji mkuu wa Russia kwa madhumuni ya kufanya mazungumzo ya mashauriano na kubadilishana mawazo na viongozi wa Moscow kuhusu mchakato wa amani wa nchi yake na masuala ya kikanda.
-
Rais Putin: Ugaidi ni tishio hatari zaidi kwa dunia
Feb 25, 2021 12:14Rais Vladimir Putin wa Russia amesema nchi yake itaendeleza vita dhidi ya ugaidi katika maeneo ya mbali kama vile Syria na kuongeza kuwa: "Ugaidi ni tishio hatari zaidi kwa dunia."
-
Admeri Khanzadi: India itajiunga na mazoezi mseto ya kijeshi ya Iran na Russia katika Bahari ya Hindi
Feb 17, 2021 02:26Kamanda wa Jeshi Majini la Jamhuri ya Kiislamu ya Iran amesema lengo kuu la mazoezi mseto ya usalama wa baharini katika eneo la kaskazini mwa Bahari ya Hindi ni kufikia usalama jumla kieneo. Aidha ameongeza kuwa, Jeshi la Majini la India sasa litajiunga na majeshi ya majini ya Iran na Russia katika mazoezi hayo.
-
Russia yatishia kukata uhusiano na Umoja wa Ulaya iwapo itawekewa vikwazo vipya
Feb 12, 2021 11:45Waziri wa Mambo ya Nchi za Nje wa Russia amesema kuwa nchi hiyo iko tayari kukata uhusiano wake na Umoja wa Ulaya iwapo itawekewa vikwazo zaidi vinavyotishia uchumi wake kutokana na mizozo inayoendelea baina ya pande hizo mbili baada ya kufungwa jela mpinzani wa serikali ya Moscow, Alexei Navalny na ukandamiza wa maandamano yaliyoanzishwa na waungaji mkono wake.
-
Zakharova: Moscow itachapisha nyaraka za kuhusika nchi za Magharibi katika machafuko ya Russia
Feb 12, 2021 02:41Msemaji wa Wizara ya Mashauri ya Kigeni ya Russia amesema kuwa, nchi hiyo ina azma ya kuzitumia jumuiya za kimataifa nyaraka na ushahidi wa kuhusika nchi za Magharibi katika machafuko na maandamano haramu katika miji mbalimbali ya nchi.
-
Qalibaf: Iran na Russia zinatafakari kuhusu ushirikiano wa miaka 20 na 50 ijayo
Feb 10, 2021 13:13Spika wa Majlisi ya Ushauri ya Kiislamu, Bunge la Iran, amesema Iran na Russia zinatafakari kuhusu ushirikiano wa kipindi cha miaka 20 na 50 ijayo.
-
Ulyanov: Makubaliano ya nyuklia ya JCPOA yarejee katika hali ya kabla ya serikali ya Trump
Feb 10, 2021 06:44Mwakilishi wa Russia katika jumuiya za kimataifa mjini Vienna amesema kuwa, ili kuweza kuhuisha makubaliano ya nyuklia ya JCPOA kuna ulazima wa serikali ya Marekani kurejea katika hali iliyokuwepo kabla ya serikali iliyoondoka madarakani ya Donald Trump bila ya masharti yoyote na kisha pande mbili za Marekani na Iran zitekeleze majukumu yao kwa mujibu wa makubaliano hayo na kufutwa vikwazo vyote vilivyowekwa dhidi ya Iran.