-
Matokeo ya karibuni ya uhesabuji kura za awali katika uchaguzi wa bunge Lebanon
May 16, 2022 07:37Ripota wa televisheni ya al Aalam ametangaza kuwa, Harakati ya Amal inayoongozwa na Nabih Berri Spika wa Bunge la Lebanon imetangaza baada ya kujulikana matokeo ya awali ya uhesabuji kura kwamba, hadi sasa imeshinda viti 17 bungeni huku Harakati ya Muqawama ya nchi hiyo Hizbullah pia ikishinda viti 23 hadi sasa.
-
Duru ya pili ya uchaguzi Ufaransa; mchuano baina ya Macron na Le Pen
Apr 12, 2022 11:04Uchaguzi wa Rais nchini Ufaransa umemalizika huku Emmanuel Macron na Marine Le Pen wakiingia katika duru ya pili. Kwa utaratibu huo, siku 14 zijazo yaani tarehe 24 mwezi huu hatima ya uchaguzi huo itajulikana na mshindi wa duru hiyo atapata tiketi ya kuingia katika ikulu ya Elizeh.
-
Tarehe mpya ya Uchaguzi wa Rais nchini Libya
Jan 05, 2022 10:01Tume ya Taifa ya Uchaguzi ya Libya imetangaza tarehe 24 mwezi huu wa Januari 2022 kuwa siku ya kufanyika uchaguzi wa rais nchini humo licha ya kwamba bado kuna hitilafu kuhusu wakati hasa unaopaswa kufanyika uchaguzi huo.
-
Kuendelea mivutano ya uchaguzi huko Libya
Dec 13, 2021 04:30Katika kipindi hiki cha kukaribia wakati wa kufanyika uchaguzi huko Libya, mivutano ya kisiasa imepamba moto nchini humo kwa kadiri kwamba, Tume Kuu ya Uchaguzi ya nchi hiyo imetangaza habari kuakhirishwa zoezi la kuchapisha orodha ya mwisho ya wagombea wa kiti cha urais.
-
Mwana wa kiume wa Muammar Gaddafi akataliwa kugombea urais
Nov 25, 2021 08:03Tume ya Taifa ya Uchaguzi ya Libya imewakatalia shakhsia 25 akiwemo Saiful Islam Gaddafi mwana wa kiume wa kiongozi wa zamani wa Libya Kanali Muammar Gaddafi kugombea uchaguzi ujao wa rais nchini humo.
-
Vikwazo vipya vya Marekani dhidi ya Iran kwa kisingizio cha kuingilia uchaguzi
Nov 20, 2021 13:43Wizara ya Fedha ya Marekani juzi Alhamisi ilitangaza kuwa imeyaweka katika orodha yake ya vikwazo majina ya shakhsia sita na shirika moja la Iran kwa kisingizio cha kuingilia uchaguzi wa rais wa Marekani. Ofisi inayosimamia fedha ya taasisi hiyo ya Marekani imesema kuwa imeyaweka katika orodha yake ya vikwazo majina ya watu sita na taasisi moja ya Iran kwa kile ilichokitaja kuwa kujaribu kuathiri uchaguzi wa rais wa Marekani wa mwaka 2020.
-
Kuanza zoezi la uandikishaji wa wagombea Urais na Ubunge katika uchaguzi wa Libya
Nov 09, 2021 07:47Hatimaye baada ya miezi kadhaa ya mazungumzo na vuta nikuvute baina ya makundi na mirengo tofauti ya kisiasa nchini Libya, uandikishaji majina ya wagombea wa kiti cha urais na Bunge ulianza Jumatatu ya jana tarehe 8 Novemba.
-
Uchaguzi muhimu wa Jumapili ya leo na mustakbali wa Ujerumani
Sep 26, 2021 04:33Leo Jumapili Wajerumani wanashiriki katika uchaguzi muhimu wenye ushindani mkali ambao ni nadra sana kuonekana katika chaguzi ziizofanyika nchini humo.
-
Bunge la Libya lapiga kura ya kutokuwa na imani na Baraza Kuu la Serikali ya nchi hiyo
Sep 23, 2021 04:13Bunge la Libya limepiga kura ya kutokuwa na imani na Baraza Kuu la Serikali ya nchi hiyo. Hatua hiyo imecukuliwa huku pande zote zinazozozana nchini Libya zikiwa mbioni kutayarisha mazingira mwafaka ya kuitisha uchaguzi huru na wa haki nchini humo na kukomesha mgogoro unaoendelea kwa zaidi ya miaka 10 sasa katika nchi hiyo ya Kaskazini mwa Afrika.
-
Mfumo wa kupiga kura kwa njia ya elektroniki nchini Russia wahujumiwa na wadukuzi
Sep 18, 2021 08:12Mwenyekiti wa Kamisheni ya Ulinzi wa Haki ya Kujitawala ya Baraza la Seneti la Russia ametangaza kuwa, mfumo wa kupiga kura kwa njia ya elektroniki nchini humo umehujumiwa na wadukuzi kutoka nchi za Magharibi.