-
Bunge la Ulaya latahadharisha kuhusu njama za Israel za kutwaa Ukingo wa Magharibi
Mar 02, 2021 10:42Wabunge wa Bunge la nchi 22 za Ulaya wameutaka Umoja wa Ulaya kuzuia mikakati ya utawala ghasibu wa Israel ya kutaka kulikalia kwa mabavu na kulitwaa eneo la Ukingo wa Magharibi huko Palestina.
-
Khatibzadeh: Huu si wakati mwafaka wa kuitishwa kikao cha JCPOA
Mar 01, 2021 03:14Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nchi za Nje wa Iran amesema kuwa, kwa kutilia maanani misimamo na hatua za karibuni za nchi tatu za Ulaya na Marekani, Jamhuri ya Kiislamu ya Iran inaona kuwa huu si wakati mwafaka wa kufanyika kikao kisicho rasmi kilichopendekezwa na Mkuu wa Siasa za Nje za Umoja wa Ulaya baina ya nchi hizo na Tehran kuhusu kadhia ya mapatano ya nyuklia ya JCPOA.
-
Sisitizo la kusimama kidete Venezuela mbele ya vita vya kiuchumi vya Marekani na Ulaya
Feb 26, 2021 12:04Kutokana na kuendelea sera za vikwazo za Marekani na madola ya Ulaya, dhidi ya Venezuela, Rais Nicolas Maduro wa nchi hiyo amesisitiza kuwa, nchi yake itaendelea kusimama kidete mkabala wa sera hizo ambazo amesema kuwa ni “vita vya kiuchumi vya pande kadhaa”.
-
Umoja wa Ulaya wakerwa na usimamishwaji wa protokali ziada ya NPT
Feb 26, 2021 07:50Umoja wa Ulaya umetoa taarifa ukibainisha kutoridhishwa kwake na uamuzi wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran wa kuanza kutekeleza sheria iliyopitishwa na Majlisi ya Ushauri ya Kiislamu (Bunge) kwa ajili ya kusimamisha utekelezaji wa protokali ziada ya mkataba wa NPT.
-
Borrell akiri kuwa Iran inafungamana na mapatano ya JCPOA na kwamba Ulaya ndio inayoyakiuka
Feb 24, 2021 11:38Baada ya kujiondoa Marekani katika mapatano ya nyuklia ya JCPOA, Umoja wa Ulaya na Troika ya Ulaya (Ujerumani, Ufaransa na Uingereza) zimekuwa na utendajikazi hasi katika uga wa kulinda mapatano hayo na pia katika kutekeleza ahadi zao. Hii ni Katika hali ambayo Iran imetekeleza ahadi zake kikamilifu katika mapatano ya JCPOA. Hivi sasa afisa wa ngazi za juu wa sera za kigeni katika Umoja wa Ulaya amekiri ukweli huo.
-
Caracas yajibu vikwazo vya Marekani na waitifaki wake dhidi ya Venezuela
Feb 23, 2021 13:10Viongozi wa Caracas wamelaani "vita vya kiuchumi vya pande kadhaa" za Umoja wa Ulaya na Marekani dhidi ya Venezuela.
-
Russia yatishia kukata uhusiano na Umoja wa Ulaya iwapo itawekewa vikwazo vipya
Feb 12, 2021 11:45Waziri wa Mambo ya Nchi za Nje wa Russia amesema kuwa nchi hiyo iko tayari kukata uhusiano wake na Umoja wa Ulaya iwapo itawekewa vikwazo zaidi vinavyotishia uchumi wake kutokana na mizozo inayoendelea baina ya pande hizo mbili baada ya kufungwa jela mpinzani wa serikali ya Moscow, Alexei Navalny na ukandamiza wa maandamano yaliyoanzishwa na waungaji mkono wake.
-
EU yapinga bomoabomoa ya nyumba za raia wa Palestina inayofanywa na Israel
Feb 10, 2021 07:03Msemaji wa Mkuu wa Siasa za Nje wa Umoja wa Ulaya (EU) ametoa taarifa akipinga vikali operesheni ya kuboa nyumba za raia wa Palestina inayofanywa na utawala wa Kizayuni wa Israel.
-
EU: Diplomasia ichukue nafasi ya mashinikizo ya kiwango cha juu
Feb 05, 2021 11:48Mkuu wa Sera za Nje wa Umoja wa Ulaya amesema 'diplomasia ya kiwango cha juu' inapaswa kuchukua nafasi ya 'mashinikizo ya kiwango cha juu.'
-
EU na US kufanya mkutano wa kujaribu kuinusuru JCPOA
Jan 29, 2021 07:49Waziri wa Mambo ya Nje wa Ujerumani amesema mazungumzo baina ya nchi za Ulaya na Marekani kuhusu kurejea Washington katika makubaliano ya nyuklia ya Iran yataanza hivi karibuni.