-
Malalamiko ya wanawake dhidi ya Trump na mustakbali wa rais huyo wa Marekani
Oct 19, 2020 06:17Katika siku zilizopita, wanawake nchini Marekani walifanya maandamano katika majimbo mbalimbali ya nchi hiyo likiwemo la Washington ili kutangaza upinzani wao kwa siasa za rais wa nchi hiyo, Donald Trump. Shabaha ya maandamano hayo ilikuwa ni kupinga ubaguzi wa rangi na ukandamizaji dhidi ya wanawake. Waendeshaji wa maandamano hayo waliahidi kuendelea na operesheni hiyo waliyoipa jina la maandamano 429 katika mikoa 50 ya Marekani.
-
Pakistan yamkamata mtuhumiwa wa pili baada ya mwanamke kubakwa na genge la watu
Oct 14, 2020 02:24Mshukiwa wa pili amewekwa kizuizini nchini Pakistan baada ya kukamatwa na polisi kufuatia ubakaji wa genge la watu dhidi ya mwanamke mmoja ambao umeibua maandamano kote nchini humo.
-
UN: Thuluthi moja ya wanawake wanakabiliwa na dhulma za kijinsia
Nov 25, 2019 12:12Umoja wa Mataifa umesema katika kila wanawake watatu, mmoja amekabiliwa na dhulma za kijinsia au kunajisiwa.
-
UNFPA yataka dhuluma dhidi ya wanawake katika jamii zikomeshwe
Nov 14, 2019 14:28Mmoja kati ya wanawake watatu duniani hukumbana na dhuluma za kijinsia kutoka kwa wapenzi au waume zao.
-
Ramaphosa atangaza mpango wa kuwalinda wanawake wa Afrika Kusini
Sep 20, 2019 02:27Rais Cyril Ramaphosa wa Afrika Kusini ametangaza sababu zilizomfanya aitishe kikao maalumu cha Bunge akisisitiza kuwa, mgogoro wa kuteswa na kunyanyaswa kupindukia wanawake nchini humo ndiko kulikomlazimisha aitishe kikao hicho.
-
Umaarufu wa Trump wazidi kupungua kote Marekani
Aug 31, 2019 16:08Umaarufu wa Rais Donald Trump wa Marekani unazidi kupungua kwa kasi nchini humo huku uchaguzi mkuu wa 2020 ukikaribia. Kwa mujibu wa uchunguzi wa maoni uliofanyika hivi karibuni, umaarufu wa Trump umepungua miongoni mwa wanawake wa Marekani.
-
Independent: Wanawake wamepuuzwa katika mfumo mpya wa utawala Sudan
Aug 05, 2019 12:12Gazeti la Independent linalochapishwa nchini Uingereza limendika kuwa, mfumo mpya wa utawala nchini Sudan umepuuza nafasi na mchango mkubwa wa wanawake katika mapinduzi yaliyouondoa madarakani utawala wa aliyekuwa rais wa nchi hiyo, Omar al Bashir.
-
Zaidi ya nusu ya wanawake nchini Morocco wanakabiliwa na ukatili
May 16, 2019 06:31Uchunguzi rasmi uliotangazwa nchini Morocco unaonyesha kwamba, zaidi ya nusu ya wanawake wa nchi hiyo wanakumbwa na ukatili dhidi yao.
-
Tanzania yatakiwa kuangalia upya sheria zinazokandamiza wanawake
Mar 08, 2019 07:58Huku Tanzania ikijiunga na nchi nyingine duniani katika maadhimisho ya Siku ya Wanawake inayoadhimishwa hii leo, serikali ya Dar es Salaam imetakiwa kuangalia upya sera na sheria zinazohusu wanawake ili kuimarisha ustawi wao.
-
Wanawake Wapalestina wanaoshikiliwa katika jela za Israel wanadhalilishwa kijinsia na kuteswa
Nov 29, 2018 03:09Wanawake Wapalestina ambao wameingizwa hivi karibuni katika jela ya utawala haramu wa Kizayuni ya Hasharon, katika eneo la Al-Damun, wamesema kwamba wanakabiliwa na mateso makubwa na kutusiwa huku haki yao ya kupatiwa huduma za kiafya ikipuuzwa na utawala huo.