-
Iran kuzalisha kilo 9 za urani iliyorutubishwa kwa 20% kwa mwezi
Jan 06, 2021 04:42Mkuu wa Shirika la Nishati ya Atomiki la Iran (AEOI) Ali Akbar Salehi amesema kuanzia sasa Jamhuri ya Kiislamu itakuwa inazalisha kilo tisa za urani iliyorutubishwa kwa kiwango cha asilimia 20 kila mwezi.
-
Mkuu wa IAEA: Iran inataka kuona dunia yenye usalama na uthabiti
Dec 17, 2020 07:38Mkurugenzi Mkuu wa Wakala wa Kimataifa wa Nishati ya Atomiki (IAEA) amesema hamu kubwa ya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran ni kuona usalama na uthabiti vinatawala duniani kote, na kwamba Tehran iko tayari kufanya mazungumzo amilifu na mataifa ambayo yapo tayari kufuata njia ya mazungumzo.
-
Iran yataka Baraza la Usalama la UN lichunguze mauaji ya Fakhrizadeh
Nov 29, 2020 12:20Naibu Waziri wa Sheria wa Iran ametoa wito kwa Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa kuchunguza mauaji ya mwanasayansi wa nyuklia wa Iran shahidi Mohsen Fakhrizadeh.
-
Russia kuanzisha kambi ya jeshi nchini Sudan, itakuwa na meli za nyuklia
Nov 12, 2020 10:14Serikali ya Russia imechapisha hati ya makubaliano yake ya Sudan yanayoiruhusu Moscow kujenga kambi ya kijeshi na misaada ya kilojestiki ya jeshi la majini la nchi hiyo nchini Sudan ambacho kitakuwa na askari na maafisa 300 wa kijeshi.
-
UN yatangaza kuanza kutekelezwa mkataba wa kuzuia silaha za nyuklia
Oct 25, 2020 08:03Umoja wa Mataifa umetangaza kuwa nchi nyingine 50 zimepasisha utekelezaji wa mkataba unaopiga marufuku silaha za nyuklia.
-
Kukiri mshauri wa usalama wa taifa wa Marekani malengo halisi ya Washington dhidi ya Iran
Oct 19, 2020 02:30Tarehe 8 Mei 2018 Marekani chini ya utawala wa Donald Trump, ilijitoa kwenye mapatano ya kimataifa ya nyuklia ya JCPOA na kuiwekea Iran vikwazo vikubwa zaidi ambavyo havijawahi kutokea. Ijapokuwa awali serikali ya Trump ilidai kuwa inataka mapatano ya nyuklia ya JCPOA yaangaliwe upya ndio maana imejitoa kwenye makubaliano hayo, lakini hivi sasa inatangaza waziwazi lengo lake hasa la kujitoa kwenye mapatano hayo.
-
Onyo la Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa kuhusu hatari ya kutokea maafa ya nyuklia duniani
Oct 05, 2020 07:05Kuongezeka maghala ya silaha za nyuklia na mashindano ya kuboresha silaha hizo ni jambo linalohatarisha usalama wa dunia, suala ambalo limeupelekea Umoja wa Mataifa kutangaza wazi wasiwasi wake kuhusiana na hatari hiyo.
-
Gharib Abadi: Shughuli za nyuklia za Iran zina uwazi zaidi kuliko za nchi nyingine zote wanachama wa IAEA
Sep 17, 2020 13:16Balozi na mwakilishi wa kudumu wa Iran katika mashirika ya kimataifa yenye makao yao mjini Vienna amesema asilimia 22 ya ukaguzi wote uliofanywa duniani na Wakala wa Kimataifa wa Nishati ya Atomiki IAEA imefanyiwa Iran na akaeleza kwamba Tehran ndiyo inayoendesha kwa uwazi zaidi shughuli zake za nyuklia zenye malengo ya amani kuliko nchi zote wanachama wa wakala huo.
-
Msimamo wa kukinzana wa Marekani kuhusu mgogoro wa nyuklia wa Korea
Aug 28, 2020 10:12Takriban ni miongo 7 sasa ambapo Marekani ina wanajeshi wake katika Rasi ya Korea. Licha ya kufanyika mazungumzo mara kadhaa baina ya viongozi wa Marekani na Korea Kaskazini kuhusu kupokonywa silaha za nyuklia Pyongyang lakini mgogoro wa Korea mbili bado uko vile vile. Si hayo tu lakini rais wa Marekani, Donald Trump hivi sasa anataka kupunguzwa idadi ya wanajeshi wa nchi hiyo huko Korea Kusini, suala ambalo limezusha mzozo mpya.
-
Zarif: Safari ya Mkuu wa IAEA Iran haina uhusiano na 'Snapback Mechanism'
Aug 24, 2020 11:59Waziri wa Mambo ya Nchi za Nje wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran amesema safari ya Mkurugenzi Mkuu wa Wakala wa Kimataifa wa Nishati ya Atomiki (IAEA), Rafael Grossi hapa nchini haina mfungamano wowote na utaratibu wa kurejesha vikwazo vya Umoja wa Mataifa dhidi ya Iran unaofahamika kama 'Snapback Mechanism'.