Feb 28, 2018 16:28 UTC
  • Mogherini ataka kuandaliwa mazingira ya kusimamisha vita kote nchini Syria

Mkuu wa Siasa za Nje wa Umoja wa Ulaya ameziomba Russia, Iran na Uturuki ziandae mazingira ya kusimamisha mapigano huko Syria.

Federica Mogherini ametuma barua tofauti kwa Mawaziri wa Mambo ya Nje wa Russia, Iran na Uturuki na bila ya kuashiria uungaji mkono wa moja kwa moja na usio wa moja kwa moja wa nchi za Magharibi kwa magaidi huko Syria, amewataka mawaziri hao kuchukua hatua za dharura kwa ajili ya kusimamisha mapigano, kuwalinda na kuwasaidia raia wa Syria na vile kuandaa mazingira ya kutuma haraka misaada ya kibinadamu nchini humo na kuwapatia matibabu majeruhi na waathiriwa wa mapigano. 

Federica Mogherini, Mkuu wa Siasa za Nje wa Umoja wa Ulaya 

Mogherini amezitaka pia pande husika katika mazungumzo ya amani ya Syria huko Astana, Kazakhstan kutayarisha mazingira ya kusitisha mapigano nchini Syria katika kipindi kisichopungua siku 30.

Katika barua aliyowatumia pia Mawaziri wa Mambo ya Nje wa nchi 28 wanachama wa Umoja wa Ulaya na vilevile kwa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, Mkuu wa Siasa za Nje wa Umoja wa Ulaya ameeleza kuwa, kuandaliwa mazingira ya usitishaji vita kunatayarisha fursa ya kusonga mbele mazungumzo ya amani yanayosimamiwa na Umoja wa Mataifa.

Umoja wa Ulaya unatazamia kuitisha mkutano wa kimataifa kuhusu Syria tarehe 25 na 26 mwezi Aprili mwaka huu. 

Tags

Maoni