Sep 11, 2019 12:11 UTC
  • Abdullah Abdullah: Maadui wa Afghanistan wanaulenga umoja wa Waislamu wa Shia na Suni

Mkuu wa Baraza la Utekelezaji la Serikali ya Umoja wa Kitaifa nchini Afghanistan, Abdullah Abdullah amesema kuwa, umoja wa Waislamu wa Shia na Suni unalengwa na maadui.

Abdullah Abdullah, ameyasema hayo katika marasimu ya kumbukumbu za Siku ya Ashura mjini Kabul, mji mkuu wa Afghanistan na kuongeza kuwa, siku ya Ashura ni dhihirisho la umoja wa Shia na Suni. Amesisitiza kuwa licha ya maadui kufanya njama kubwa zenye lengo la kuibua tofauti kati ya wananchi, lakini raia walio macho wa Afghanistan wameendelea kuhuisha siku hiyo.

Machafuko nchini Afghanistan

Aidha Mkuu wa Baraza la Utekelezaji la Serikali ya Umoja wa Kitaifa nchini Afghanistan ameongeza kwamba kwa kutumia uelewa na hisia za juu katika uga wa kisiasa, raia wa nchi hiyo wamefanikiwa kusambaratisha njama za maadui wa Uislamu. Ameongeza kuwa, kwa baraka za mwezi huu wa Muhharram anatumai raia wa Afghanistan watafikia amani kamili ambapo sambamba na kufanyika uchaguzi wa kiuadilifu, wataweza kuishi kwa usalama na amani nchini humo.

Maoni