Sep 11, 2019 12:19 UTC
  • Radiamali zatolewa kufuatia kutimuliwa ghafla John Bolton katika ikulu ya White House

Kitendo cha kupigwa kalamu nyekundu na Rais Donald Trump, John R. Bolton, Mshauri wa Usalama wa Taifa wa Marekani, kimeendelea kuakisiwa kwa radiamali tofauti na viongozi wa Marekani.

Jana Rais Donald Trump alitoa ujumbe kwenye mtandao wa kijamii wa Twitter akisema kuwa, Bolton, Mshauri wake wa Usalama wa Taifa, hafai tena kuwa kwenye serikali yake na kwamba ifikapo wiki ijayo atakuwa amemtangaza mshauri wake mwingine. Katika uwanja huo, Hogan Gidley mmoja wa wasaidizi wa Trump amenukuliwa akisema kuwa, kwa sasa Charles Copeman ndiye ameshikilia kwa muda nafasi ya usalama wa taifa katika ikulu ya White House. Hii ni katika hali ambayo Bolton ameandika katika mtandao wa Twitter kufuatia hatua ya ghafla ya Trump dhidi yake na pia kusambaratika kwa mpango unaoitwa timu (B) kwamba: "Mimi nilikuwa nimewasilisha ombi la kujiuzulu, ambapo Trump aliniambia nisubiri tutalizungumzia suala hilo kesho."

Bolton wakati alipokuwa katika ikulu ya White House

Kufuatia mgongano huo kati ya Trump na Bolton, akijibu swali aliloulizwa iwapo amepatwa na mshangao baada ya kupigwa kalamu nyekundu mkuu huyo wa zamani wa usalama wa taifa, Waziri wa Fedha wa Marekani, Steven Mnuchin sambamba na kucheka, amesema kuwa, mtazamo wa Trump kuhusiana na vita vya Iraq, ulikuwa unatofautiana na ule wa John Bolton. Kwa upande wake, Rand Paul Seneta wa chama cha Republican pia, amesema: "Tishio la kutokea vita duniani, limepungua, sambamba na kuondoka Bolton katika ikulu ya Marekani." Aidha Bob Menendez, Seneta wa jimbo la New Jersey ambaye pia ni mjumbe wa kamati ya uhusiano wa kigeni katika bunge la seneti nchini humo kupitia mahojiano na kanali ya CNN amesema kuwa, John Bolton amepigwa kalamu nyekundu kutokana na kutokuwa na taathira katika siasa za kigeni na usalama wa taifa wa nchi hiyo. 

Tags

Maoni