Sep 28, 2019 08:04 UTC
  • Nchi nane za dunia zaunga mkono tangazo la usitishaji vita la Answarullah ya Yemen

Wajumbe wa kudumu katika Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa pamoja na Ujerumani, Kuwait na Sweden, zimeunga mkono tangazo la usitishaji vita la Harakati ya Kiislamu ya Answarullah nchini Yemen.

Taarifa iliyotolewa na nchi hizo, imesema kuwa ubunifu wa harakati hiyo kwa ajili ya kusimamisha mashambulizi yake, ni hatua muhimu yenye lengo la kupunguza mzozo, na ambayo pia ni hatua nyingine chanya na inayohitajika kutoka kwa Answarullah. Aidha taarifa hiyo imeutaka muungano vamizi wa Saudia kukubali tangazo hilo. Taarifa hiyo pia imeashiria matokeo ya hivi karibuni katika mkoa wa Aden, kusini mwa Yemen na kubainisha kuwa matukio hayo yanabainisha udharura wa kuanzishwa haraka mchakato jumla wa kisiasa ambao utapelekea kuhitimishwa mapigano katika mkoa huo.

Jinai na uharibifu wa kutisha wa Saudia dhidi ya raia madhlumu wa Yemen

Katika uwanja huo, Ijumaa ya tarehe 20 mwezi huu, Mahdi al-Mashat, Mkuu wa Baraza Kuu la Kisiasa nchini Yemen alinukuliwa akisema kuwa mashambulizi ya Wayemen ya ndege zisizo na rubani na makombora dhidi ya Saudia yatakomeshwa kwa masharti na kuongeza kuwa Yemen inataraji kuwa hatua hiyo itapokelewa kwa jibu chanya na muungano vamizi wa Saudia. Kwa upande wake, Mohammed Ali al-Houthi, Mkuu wa Kamati Kuu ya Mapinduzi  ya Yemen pia amesisitizia umuhimu wa kuungwa mkono ubunifu wa Mahdi al-Mashat wa kusimamishwa kikamilifu uvamizi nchini Yemen.

Tags

Maoni