Oct 22, 2019 03:17 UTC
  • Russia kuchagua sarafu mpya zitakazochukua nafasi ya dola

Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Fedha wa Russia ametangaza kuwa nchi hiyo imeanisha Euro na Yuan kuwa sarafu za kigeni itakazotumia katika miamala yake ya kifedha.

Akizungumza pambizoni mwa  Kikao cha Mfuko wa Fedha wa Kimataifa (IMF) na Benki ya Dunia huko Washington, Anton Siluanov  amesema kuwa Yuan ni sarafu ya fedha ya China na Euro ni sarafu ambazo kwa kiasi kikubwa zinaweza mwaka ujao wa 2020 kuanishwa kuwa sarafu za fedha zitakazotumika katika miamala ya dhamana na nyaraka za hisa za Russia. 

Anton Siluanov, Naibu Waziri Mkuu wa Russia ambaye pia ni Waziri wa Fedha 
 

Naibu Waziri Mkuu wa Russia ambaye pia ni Waziri wa Fedha wa nchi hiyo ameongeza kuwa, iwapo mwaka ujao wa 2020 miamala ya mikopo na malipo yake itainishwa kwa sarafu ya Euro; kiwango cha dhamana ya fedha hizo kitakuwa sawa na dola bilioni tatu.  

Kwa mujibu wa moja ya vifurushi vya vikwazo vya Marekani dhidi ya Russia ambavyo vilipasishwa mwezi Agosti mwaka huu, ununuaji wa nyaraka za hisa za Russia na kuwekeza kwenye dhamana hizo ulipigwa marufuku. 

Tags

Maoni