Oct 23, 2019 02:45 UTC
  • Baada ya kuiita 'ng'ombe mkamwa maziwa wa Marekani', Trump aidhalilisha tena Saudia

Rais Donald Trump wa Marekani ameidhalilisha tena Saudi Arabia na viongozi wake katika mahijiano yake na waandishi wa habari.

Doland Trump aliyekuwa akizungumza jana na televisheni ya Fox News ameidunisha na kuidhalilisha tena Saudi Arabia na kusema Wasaudia hawana lolote isipokuwa fedha tu. 

Amesema kuwa Saudi Arabia inailipa Marekani gharama zote za kuilinda nchi hiyo. 

Hii si mara ya kwanza kwa Doland Trump kuzungumzia suala la himaya na jinsi Marekani inavyoilinda Saudia. Awali rais huyo wa Marekani alikuwa amemtahadharisha Mfalme Salman bin Abdulaziz Al Saud wa Saudia kwamba, bila ya himaya na ulinzi wa majeshi ya Marekani hawezi kuendelea kuwepo madarakani kwa zaidi ya wiki mbili. 

Mfalme Salman bin Abdulaziz Al Saud akimvika Trump nishani ya juu Saudia

Kabla ya hapo pia rais huyo wa Marekani aliwafananisha viongozi wa Saudi Arabia na ng'ombe anayekamwa maziwa akitangaza wazi kwamba ni ulinzi wa Washington ndio unaowaweka madarakani viongozi hao wa Saudia, hivyo lazima walipe gharama za ulinzi huo.

Baada ya rais wa Marekani kuwadhalilisha hivyo viongozi wa Saudia, Dk Mohammad Javad Zarif, Waziri wa Mambo ya Nje wa Iran aliandika kwenye ukurasa wake wa Twitter kwamba "kudhalilishwa" ndiyo zawadi ya upotofu wa kutegemea ulinzi kutoka kwa wageni.

Tags

Maoni