Nov 13, 2019 07:54 UTC
  • Trump: Ni bora kufanya biashara na China kuliko Ulaya

Rais Donald Trump wa Marekani ameutuhumu Umoja wa Ulaya kwa kuweka vizuizi vya kutisha vya kibiashara.

Trump ameyasema hayo mjini New York ambapo akizitaja siasa za kibiashara za Ulaya dhidi ya Marekani kuwa ni za kibaguzi amesema kuwa, vizuizi vya kibiashara vilivyowekwa na EU ni vya kutisha na vibaya zaidi kuliko hata vya China. Ameashiria mabadilishano ya kibiashara kati ya nchi yake na nchi wanachama wa Umoja wa Ulaya na kuongeza kuwa, Marekani haiweze kuzalisha bidhaa na kuzipeleka Ulaya, katika hali ambayo EU huingiza bidhaa zake nchini Marekani tena kwa ushuru mdogo wa forodha. Akizungumzia China ambayo hadi sasa bado hajaweza kuipigisha magoti kukubali matakwa yake kuhusu ushuru wa forodha, kwa mara nyingine Trump ameonyesha matarajio kwamba hatimaye ataweza kufikia makubaliaano na serikali ya Beijing na kutiwa saini mkataba wa kibiashara baina ya nchi mbili.

Vita vya kibiashara kati ya Marekani na Umoja wa Ulaya

Tangu mwaka 2018 na kupitia madai kuwa uhusiano wa kibiashara kati ya Washington na marafiki wake sio wa kiuadilifuu na ni wenye kuidhuru Marekani, Trump alianza kutekeleza siasa hasi dhidi ya Beijing kwa kuzipandishia ushuru wa forodha bidhaa zinazozalishwa Uchina na kuingizwa Marekani. Hatua hiyo ilikabiliwa na radiamali kali ya China, ambayo nayo ilizipandishia ushuru bidhaa zinazozalishwa nchini Marekani. Matokeo ya uchunguzi kutoka jimbo la Los Angeles nchini Marekani, na ambalo ndilo lenye bandari kuu nchini humo, yanaonyesha kwamba hatua ya Washington kuzipandishia ushuru wa forodha bidhaa za nchi washirika iliyoenda sambamba na kujibiwa mapigo na nchi hizo, imehatarisha ajira za karibu watu milioni moja na nusu nchini Marekani.

Tags

Maoni