Nov 13, 2019 12:06 UTC
  • Russia yatahahadharisha kuhusu uingiliaji wa kigeni katika mgogoro wa Bolivia

Wizara ya Mambo ya Nje ya Russia imetahadharisha kuhusu athari mbaya ziinazoweza kutokea kutokana na uingiliaji wa kigeni katika mgogoro wa Bolivia.

Sergei Ryabkov, Naibu Waziri wa Mambo ya Nje wa Russia ameyataka madola makubwa kutotumia vibaya mgogoro ulioibuka nchini Bolivia.

Ryabkov amesema Russia haitaki matukio ya Bolivia yasababishe ukosefu wa usalama nchini humo. Tarehe 10 Novemba, Rais Evo Morales wa Bolivia alilazimika kujiuzuluu kutokana na mashinikizo ya wapinzani wake wanaosaidiwa na kuungwa mkono na Marekani na jeshi la nchi hiyo. Morales amekubali kwenda uhamishoni nchini Mexico. 

Wakuu wa Marekani wametangaza kuunga mkono machafuko ya Bolivia ambayo yamepelekea kulazimishwa Morale kuondoka madarakani.

Sergei Ryabkov

Wakati huo huo,  Morales amesisitiza kwamba alilazimika kuchukua hatua hiyo kutokana na mashinikizo na kwamba ataendeleza mapambano yake.

Morales ambaye ameyasema hayo baada ya kuwasili nchini Mexico hapo siku ya Jumanne amebainisha kwamba kumefanyika mapinduzi dhidi yake na kuongeza kuwa, mashinikizo makali ndiyo yamemfanya ajiuzulu uongozi. Amesema kuwa, hatua ya serikali ya Mexico kumpokea, imeokoa maisha yake. Akiashiria njama za wapinzani wake za kutaka kumuua, ameishukuru serikali ya Mexico kwa kumpokea na kusisitiza kuwa, ataendeleza mapambano yake ya kisiasa kwa muda wote atakaokuwa hai.

Maoni