Nov 13, 2019 13:32 UTC
  • Waislamu Uingereza waanzisha oparesheni ya kumtimua Boris Johnson

Kundi moja la Waislamu Uingereza limeanzisha kampeni mpya inayojulikana kama "Oparesheni ya Kura ya Waislamu' kuwatimua wabunge wasio zingatia maslahi yao.

Kampeni hiyo inalenga kuwahamasisha Waislamu Uingereza kujitokeza kwa wingi katika uchaguzi mkuu ujao ili kuwatimua wagombea ambao hawawatetei Waislamu. Mlengwa mkuu katika kampeni hiyo ni Waziri Mkuu Boris Johnson ambaye pia ni kiongozi wa chama cha Conservative. Johnson anatetea kiti chake katika eneo bunge la Uxbridge na South Ruislip. Johnson anatetea kiti hicho huku akichukuana na kingozi wa chama cha Leba Jeremy Corbyn katika kuwania uongozi wa Uingereza.

Kamati ya Umma ya Waislamu Uingereza imeanzisha kampeni ya kuwashajiisha Waislamu katika mitaa ya Uxbridge na Ruislip, ili wampigie kura mgombea wa chama cha Leba, Ali Milani.

Ali Milani

Inatazamiwa kuwa, iwapo Waislamu watajitokeza kwa wingi basi Johnson atapoteza kiti hicho na hivyo kutoa pigo kubwa kwa chama cha kihafidina cha Conservative. Uchaguzi mkuu Uingereza umepangwa kufanyika Disemba 12.

 

Tags

Maoni