Nov 21, 2019 01:04 UTC
  • Marekani yadai kutekeleza makubaliano na Korea Kaskazini

Wizara ya Mambo ya Nje ya Marekani imedai kwamba, Rais Donald Trump wa nchi hiyo ametekeleza makubaliano ya kuangamizwa silaha za nyuklia yaliyofikiwa kati yake na Korea Kaskazini.

Kufuatia serikali ya Korea Kaskazini kutangaza upinzani wake wa kuendelea na mwenendo wa mazungumzo yasiyo na faida na serikali ya Marekani, Wizara ya Mambo ya Nje ya nchi hiyo imetoa taarifa ikisema kuwa, Trump anafungamana na ahadi alizotoa katika kikao cha nchini Singapore. Kwa mujibu wa ripoti hiyo makubaliano hayo yanahusiana na kubadilishwa tabia, kudumishwa usalama na kuangamizwa kikamilifuu silaha za nyuklia.

Mkutano wa Trump na Kim Jong-un nchini Singapore

Hayo yanajiri katika hali ambayo viongozi wa Korea Kaskazini kwa mara kadhaa wamesema kwamba serikali ya Pyongyang haipendelei kuendelea na mazungumzo yasiyo na faida na Marekani. Makubaliano ya Singapore yalifikiwa kati ya Rais Donald Trump na Kim Jong-un, Kiongozi wa Korea Kaskazini mwezi Juni mwaka jana ambapo hata hivyo hadi sasa Washington imeshindwa kutekeleza makubaliano hayo. Jumapili iliyopita Trump aliandika katika mtandao wa kijamii akimuhutubuu Kim Jong-un, Kiongozi wa Korea Kaskazini kwamba anatakiwa kuharakisha kufikiwa makubaliano kamili kuhusiana na kuangamizwa silaha za nyuklia.

Tags

Maoni