Nov 21, 2019 11:46 UTC
  • Luxembourg: Umoja wa Ulaya unapasa kulitambua rasmi taifa la Palestina

Waziri wa Mambo ya Nje wa Luxembourg amesisitiza kwamba Umoja wa Ulaya ni lazima uitambue rasmi nchi huru ya Palestina.

Jean Asselborn ameyasema hayo katika mazungumzo na Shirika la Habari la Reuters ambapo ameongeza kwamba, kutambuliwa rasmi nchi huru ya Palestina si kuwa ni jambo la fadhila wala sio cheki nyeupe, bali kutambuliwa huko rasmi ni haki halali ya raia wa Palestina kwa ajili ya kuwa na nchi yao. Matamshi hayo ya Asselborn yamekuja ikiwa ni baada ya matamshi ya Mike Pompeo, Waziri wa Mambo ya Nje wa Marekani kutangaza Jumatatu iliyopita kubadilika siasa za Washington kuhusiana na ujenzi wa vitongoji vya walowezi wa Kizayuni katika Ukingo wa Magharibi wa Mto Jordan unaofanywa na utawala haramu wa Kizayuni na kwamba kuanzia sasa Marekani haitambui ujenzi huo wa vitongoji kuwa unakiuka sheria za kimataifa.

Licha ya ukandamizaji wa Israel lakini bado bendera ya Palestina inapepea

Matamshi hayo ya Pompeo yamelaaniwa vikali katika ngazi ya kieneo na kimataifa. Kwa mujibu wa tangazo la Umoja wa Ulaya, umoja huo pia unaamini kwamba kwa mujibu wa sheria za kimataifa, ujenzi wa vitongoji vya walowezi wa Kizayuni katika ardhi za Palestina zinazokaliwa kwa mabavu ni kinyume cha sheriia.

Tags

Maoni