Nov 21, 2019 11:53 UTC
  • Bernie Sanders: Saudia ni dikteta mmoja asiye na huruma

Bernie Sanders mmoja wa wagombea wa chama cha Democrat kwenye uchaguzi wa rais wa mwaka 2020 nchini Marekani ameutaja utawala wa kifalme wa Saudia kuwa ni 'mwitifaki aisiyeaminika.'

Sanders ameyasema hayo katika mdahalo wa uchaguzi ambapo sambamba na kusisitizia kuwa Marekani haipasi kuiamini Saudia na huku akikumbushia mauaji ya Jamal Khashoggi, mwandishi wa habari na mkosoaji wa serikali ya Riyadh, amesema: "Udikteta usio na huruma wa Aal Saud unafanya kila unaloliweza kwa ajili ya kufuta demokrasia." Kadhalika Bernie Sanders ameitaka serikali ya Washington kufanya juhudi ambazo zitafanikisha mwenendo wa mazungumzo ambayo yatalinda izza na heshima ya raia wa Palestina.

Watawala wa Saudia ambao ni madikteta

Matamshi ya mgombea huyo anayejitegemea yametolewa katika hali ambayo Marekani ilibuni mpango unaoitwa 'Muamala wa Karne' ambao unakanyaga haki za raia wa Palestina. Kwa mujibu wa mpango huo, mji wa Quds utakabidhiwa utawala bandia wa Kizayuni na wakimbizi wa Kipalestina wanaoishi katika nchi nyingine hawatakuwa na haki ya kurejea katika ardhi zao asilia, huku taifa la Palestina likibakia na ardhi ya Ukingo wa Magharibi wa Mto Jordan pamoja na Ukanda wa Gaza pekee.

Maoni