Nov 22, 2019 07:09 UTC
  • Waislamu ni waathirika wakuu wa ugaidi duniani

Asasi moja ya Ufaransa imesema Waislamu ni waathirika wakuu wa ugaidi duniani na hilo ni jambo ambalo linapaswa kufahamika vyema barani Ulaya.

Guillaume Denoix de Saint Marc, mwenyekiti wa Jumuiya ya Waathirika wa Ugaidi Ufaransa amehutubia kikao cha kimataifa cha waathirika wa ugaidi katika mji wa Nice nchini humo na kusema: "Asilimia 80 ya waathirika wa ugaidi ni Waislamu.

Marc ameendelea kusema kuwa, Waislamu ni kati ya watu wa kwanza ambao wanaathiriwa na ugaidi na kuongeza kuwa nchi za Ulaya zinapaswa kuifahamu vyema nukta hii.

Mwenyekiti wa Jumuiya ya Waathirika wa Ugaidi Ufaransa ameendelea kubaini kuwa: "Baadhi wanadhani kuwa, wanaotekeleza ugaidi ni Waislamu tu na waathirika si Waislamu. Dhana hii haina ukweli wowote kwa sababu Waislamu pia ni waathirika wa mashambulizi ya ugaidi."

Rais Macron wa Ufaransa

Waislamu wanakadiriwa kuwa asilimia 10 ya watu wote milioni 66 nchini Ufaransa na baada ya hujuma za miaka ya hivi karibuni za kigaidi nchini humo, serikali ya Paris imekuwa ikikandamiza na kuwashinikiza Waislamu kwa kisingizio cha kupambana na ugaidi. Mashinikizo dhidi ya Waislamu yamekuwa mengi sana nchini Ufaransa kiasi kwamba Umoja wa Mataifa umeikosoa serikali ya nchi hiyo kutokana an muamala wake mbovu dhidi ya Waislamu.

 

Tags

Maoni