Nov 22, 2019 14:08 UTC
  • Waislamu milioni 27 wameuawa katika 'vita dhidi ya ugaidi' vya Marekani

Msomi na mwanafikra mashuhuri wa Marekani amesema zaidi ya Waislamu milioni 27 wameuawa kutokana na vita vilivyoibuliwa na Marekani kwa kisingizio cha kupambana na ugaidi, tangu baada ya mashambulizi ya Septemba 11, 2001 hadi sasa.

Dakta Kevin Barrett, mwanaakademia maarufu wa Marekani ambaye amekuwa akifuatilia matukio ya tangu baada ya mashambulizi ya Septemba 11 amesema hayo alipohojiwa na kanali ya Press TV kuhusu ripoti mpya ya Taasisi ya Masuala ya Kimataifa ya Watson ya Chuo Kikuu cha Brown cha Marekani.

Kwa mujibu wa utafiti mpya uliofanywa na taasisi hiyo ya Marekani, Waislamu 800,000 wameuawa katika vita vya moja kwa moja vilivyoibuliwa na Marekani katika nchi za Afghanistan, Pakistan na maeneo mengine ya Mashariki ya Kati baada ya mashambulizi ya Septemba 11 mwaka 2001.

Kwa mujibu wa Dakta Berret, takwimu za utafiti huo wa Taasisi ya Masuala ya Kimataifa ya Watson ya Chuo Kikuu cha Brown cha Marekani haziakisi ukweli wa vifo vilivyotokana na vita vilivyoanzishwa na Washington baada ya mashambulizi ya Septemba 11.

Askari wa US nchini Afghanistan, miaka kadhaa baada ya kudai kuwa wamemuua Osama Bin Laden

Amesema, "Kwa mujibu wa Dakta Gideon Polya, profesa wa Sayansi wa Australia na mtaalamu wa matukio ya vifo na mauaji amewahi kusema kuwa Waislamu milioni 27 wamekuwa wahanga wa mauaji ya kizazi na mauaji ya kimbari, huku wengine milioni tano wakiuawa wakiwa kwenye matumbo ya mama zao kabla ya kuzaliwa kutokana na vita hivyo vilivyoibuliwa kwa kisingizio cha kupambana na ugaidi baada ya mashambulizi ya Septemba 11."

Maafisa wa Washington wamekuwa wakitoa simulizi na taarifa za kukinzana kuhusu tukio la Septemba 11, ambapo Wamarekani 3,000 waliuawa. Maafisa wa Marekani hadi hii leo wameshindwa kutoa maelezo ya kukinaisha kuhusu namna magaidi 19 wa kundi la al-Qaeda chini ya uongozi wa Osma Bin Laden walitekeleza mashambulizi hayo.

Tags

Maoni