Dec 07, 2019 07:24 UTC
  • Kamisheni ya JCPOA yasisitiza juu ya kulindwa makubaliano hayo

Kikao cha 14 cha Kamisheni ya Pamoja ya Makubaliano ya Nyuklia ya JCPOA kimesisitizia tena kuhusu umuhimu wa kulindwa mapatano hayo ya kimataifa na kwamba Iran imefungamana na makubaliano hayo.

Taarifa ya mwisho ya kikao hicho iliyosomwa na Katibu Mkuu wa Umoja wa Ulaya, Helga Schmid ambaye alikuwa mwenyekiti wa kikao hicho imesema, "Washiriki wanatambua (kupongeza) kufungamana kwa Iran na mapatano hayo miezi 14 baada ya Marekani kuchukua hatua ya kusikitisha ya kujiondoa kwayo. Kitendo hicho kimeifanya Iran ikose kustafidi ipasavyo na makubaliano hayo baada ya Washington kuiwekea upya vikwazo."

Washiriki wa Kikao cha 14 cha Kamisheni ya Pamoja ya Makubaliano ya Nyuklia ya JCPOA wamekaribisha kwa mikono miwili na kupongeza hatua ya nchi sita za Ulaya ya kujiunga na mfumo maalumu wa mabadilishano ya kifedha na Iran kwa jina la INSTEX. Nchi hizo ni Ubelgiji, Norway, Denmark, Uholanzi, Sweden na Finland. 

 

Trump aliiondoa Marekani katika makubaliano ya nyuklia ya JCPOA mwezi Mei mwaka 2018

Naibu Waziri wa Mambo ya Nje wa Iran katika masuala ya kisiasa, Abbas Araqchi ambaye alikuwa mwenyekiti mwenza wa kikao hicho amesema, "Wajumbe wote wameafikiana kuwa, hatua ya upande mmoja ya Marekani ya kujiondoa kwenye JCPOA, ndicho chanzo cha taharuki katika uetekelezaji wa makubaliano hayo."

Kikao hicho kimefanyika mwezi mmoja baada ya Iran kuchukua hatua ya nne ya kupunguza utekeleza wa baadhi ya vipengee vya makubaliano ya JCPOA baada ya nchi za Ulaya kushindwa kudhamini maslahi yake ndani ya makubaliano hayo. 

Tags

Maoni