Dec 07, 2019 07:34 UTC
  • Raia wa Saudia awapiga risasi watu 11 nchini Marekani

Mwanafunzi wa urubani raia wa Saudi Arabia amewafytaulia risasi watu 11 na kuua watatu miongoni mwao katika kambi ya kijeshi ya Pensacola jimboni Florida nchini Marekani.

Mark Esper, Waziri wa Ulinzi wa Marekani amesema mwanafunzi huyo alikuwa na cheo cha Luteni II katika jeshi la Saudia, na alikuwa anasomea urubani katika kambi hiyo ya jeshi nchini Marekani.

Duru za habari zimeiambia kanali ya televisheni ya CNN kuwa, raia huyo wa Saudia ambaye ametambuliwa kwa jina la Mohammad Al-Shamrani ameuawa pia katika tukio hilo.

Mkuu wa Polisi katika eneo hilo, David Morgan amesema watu 12 wamejeruhiwa kwa risasi katika tukio hilo la jana Ijumaa.

Wakati huohuo, raia sita wa Saudia wanaohusishwa na shambulizi hilo wametiwa mbaroni kwa ajili ya kusailiwa. Watatu miongoni mwao walikuwa wakirekodi tukio hilo kwa kutumia simu zao za rununu.

Mashambulizi ya Septemba 11

Rais Donald Trump ambaye amekataa kulitaja tukio hilo kuwa la kigaidi, amefanya mazungumzo ya simu na Mfalme Salman wa Saudia ambaye amesema, Riyadh inaalani vikali hujuma hiyo na eti haiakisi hisia za Wasaudia walio wengi ambao wanaipenda Marekani.

Hili sio tukio la kwanza la ugaidi kufanywa na raia wa Saudia katika ardhi ya Marekani. Septemba 11 mwaka 2001, Wasaudia walihusika katika mashambulizi ya kigaidi katika miji ya New York na Virginia, ambapo maelfu ya watu waliuawa.

Tags

Maoni