Dec 08, 2019 04:46 UTC
  • Wasaudia wasabababisha tukio jingine la kigaidi nchini Marekani

Raia mwingine wa Saudi Arabia amehusika na tukio jingine la kigaidi huko Marekani. Mohammed Saeed al Shamrani ambaye alielekea Marekani kwa ajili ya kupata mafunzo ya urubani juzi Ijumaa alifyatua risasi na kuwauwa watu watatu katika kambi ya kijeshi ya Pensacola jimboni Florida.

Kabla ya tukio hilo la kigaidi, Al Shamrani aliandika katika ukurasa wake wa Twitter kuwa na hapa ninamnukuu, "mimi napinga shari, Marekani kiujumla imegeuka na kuwa nchi ya shari; mimi siwapingi nyingi kwa sababu ni Wamarekani, bali nawachukia kwa uhuru wenu. Nyinyi kila siku mnaunga mkono jinai si dhidi ya Waislamu tu bali dhidi ya ubinadamu. Mnadhamini kifedha na kutenda jinai hizo", mwisho wa kunukuu. 

Kituo cha anga cha PENSACOLA, jimboni Florida nchini Marekani

Hata hivyo hii si mara ya kwanza kwa raia wa Saudia kutekeleza vitendo vya kigaidi katika ardhi ya Marekani. Asubuhi ya tarehe 11 Septemba mwaka 2001 raia 15 wa Saudi Arabia na watu wengine wanne waliziteka nyara ndege nne za abiria katika anga ya nchi hiyo. Hilo lilikuwa tukio kubwa zaidi la kigaidi kutokea katika historia ya Marekani. Raia hao wa Saudia aidha walishambulia minara pacha ya Kituo cha Kimataifa cha Biashara mjini New York na jengo la Wizara ya ulinzi ya nchi hiyo (Pentagon) huko Washington na kuua watu karibu 300. Tukio hilo ambalo linatajwa kufanana na shambulio lililofanywa na Wajapan katika bandari ya Pearl Disemba 7 mwaka 1941 liliwasha moto katika Mashariki ya Kati. Mamilioni ya wananchi wa Afghanistan na Iraq walilazimishwa kuwa wahanga wa hatua ya ulipizaji kisasi ya Marekani kutokana na raia wa Saudia kutekeleza mashambulizi hayo ya kigaidi nchini humo.  

Shambulio la Sptemba 11 katika jengo la Pentagon, Marekani

Pamoja na hayo, gharama ilizopasa kulipa serikali  ya Saudi Arabia kutokana na raia wake kuhusika katika mashambulizi ya kigaidi ya Septemba 11 ilikuwa ni kuwasilisha pakubwa uungaji mkono wake wa kisiasa, kisilaha, kijeshi na kivita katika eneo. Pamona na kuwa matukio ya Septemba 11 yaliibua hisia kali dhidi ya Saudia ndani ya Marekani lakini wanasiasa wa Marekani walilazimika kufumbia macho fikra hizo za kigaidi za Wasaudia kutokana na haja yao kubwa kwa mafuta ya nchi hiyo. 

Hatua za kupenda kujitanua na mabavu za viongozi wa Marekani kwa mara nyingine tena zimewatia raia wa nchi hiyo katika hatari ya ugaidi mpya wa baadhi ya raia wa Saudia. Hii ni katika hali ambayo serikali  ya sasa na za zamani za Marekani zimeendelea kuwa bega kwa bega na kutekeleza jitihada mbalimbali za kuiunga mkono serikali ya Saudi Arabia. Mfano mmoja wa uungaji mkono huo wa wazi wa Marekani kwa Saudia, ni hatua ya Rais Donald Trump ya kufanya ziara ya kwanza nje ya nchi huko Riyadh baada ya kuingia madarakani; ambapo alisaini na viongozi wa Saudia makubaliao yenye thamani ya dola bilioni 450 ukiwemo mkataba wa silaha wa dola bilioni 110. 

Aidha wakati yalipopamba moto mashinikizo ya kimataifa dhidi ya Riyadh kufuatia mauaji ya Jamal Khashoggi mwandishi habari mkosoaji wa utawala wa Aal Saud Trump binafsi aliingilia kati suala hilo na kuizuia kongresi ya Marekani kuidhinisha vikwazo  dhidi ya Saudia. Kwa kuzingatia rekodi hiyo chafu ya Trump ni wazi kuwa kujiri ufyatuaji risasi huo wa mwanachuo wa Kisaudia dhidi ya raia wa Marekani katika kambi ya kijeshi nchini Marekani hakutaathiri uhusiano wa Washington na Saudi Arabia. 

Jamal Khashoggi, mwandishi habari aliyeuliwa na utawala wa Aal Saud

Baada ya tukio hilo, Trump amemnukuu Mfalme wa Saudi Arabia akisema kuwa: Wananchi wa Saudia wanawapenda wenzao wa Marekani.  Pamoja na hayo, wananchi wa Marekani wamegharimika zaidi  kifedha na  kupoteza watu wengi kuliko nchi nyingine yoyote katika miaka 20 ya karibuni kutokana na kukita mizizi kwa fikra za uchupaji mipaka na za kigaidi za Wasaudia.  

Maoni