Jan 14, 2020 06:50 UTC
  • Liverpool FC yawatetea Wapalestina, yakataa udhamini wa Puma kutokana na ushirikiano wake na Israel

Klabu ya soka ya Uingereza, Liverpool imekataa ufadhili wa kifedha wa kampuni ya Puma ikipinga ushirikiano wa kampuni hiyo na utawala haramu wa Israel. Liverpool imechukua hatua hiyo kutokana na mashinikizo ya mashabiki wa klabu hiyo wanaopinga mauaji na ukatili unaofanywa na Israel dhidi ya raia wasio na hatia wa Palestina.

Kutokana na mashinikizo ya mashabiki wake, klabu ya Liverpool imekatisha ufadhili na udhamini wa kampuni ya Puma ya Ujerumani kwa sababu ya ushirikiano wake wa utawala wa Kizayuni wa Israrel.

Mashabiki wa klabu ya Liverpool walisisitiza kuwa, kutokana na ushirikiano wa kifedha wa Puma na Wazayni wa Israel, wakurugenzi wa timu hiyo ya mpira wa miguu ya Uingereza wanapaswa kusimamisha udhamini wa Puma wa kutengeneza jezi, soksi na vifaa vingine vya michezo vya klabu hiyo.

Jumuiya ya Kuonesha Mshikamano na Wapalestina (PSC) imewapongeza mashabiki wa klabu ya Liverpool FC na kuwataka mashabiki wa timu nyingine zinazotumia bidhaa za kampuni ya vifaa vya michezo ya Puma kuchukua hatua kama hiyo. 

Jumuiya hiyo pia imewataka watu kote dunia kususia bidhaa za kampuni ya Puma katika jitihada zao za kuwaunga mkono na kuwatetea raia wa Palestina na kupinga jinai zinazofanywa na Israel dhidi ya watu hao. 

Susia bidhaa za Puma

Kampuni ya Ujerumani ya Puma ndiyo mdhamini mkubwa wa Federesheni ya Mpira wa Miguu ya utawala wa Kizayuni wa Israel. 

Kampuni ya vifaa vya michezo ya Adidas pia awali ikuwa mdhamini wa Wazayuni wa Israel lakini ililazimika kukata ushirikiano wake na Israel baada ya mashinikizo makubwa ya taasisi na jumuiya za kimataifa zinazopinga uhalifu na jinai za Israel huko Palestina.      

Tags

Maoni