Jan 19, 2020 02:57 UTC
  • Mexico yatupilia mbali tuhuma za Marekani dhidi ya Iran

Wizara ya Mambo ya Nje ya Mexico imetupilia mbali madai ya hivi karibuni ya gazeti la Kimarekani la Wall Street Journal kuhusiana na upenyaji wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran katika eneo la Amerika ya Latini.

Taarifa iliyotolewa kwa pamoja na Wizara ya Mambo ya Nje ya Mexicpo pamoja na ubalozi wa Iran mjini Mexico City imekadhibisha makala ya gazeti hilo. Hivi karibuni gazeti la Wall Street Journal la Kimarekani lilichapisha makala ambayo ilidai uwepo wa Iran katika eneo la Amerika ya Latini, madai ambayo yametolewa kwa lengo la kuhalalisha jinai za Washington za kumuua kigaidi Luteni Jenerali Qassem Soleimani, Kamanda wa Kikosi cha Quds cha Jeshi la Walinzi wa Mapinduzi ya Kiislamu ya Iran IRGC. Katika kujibu tuhuma hizo Wizara ya Mambo ya Nje ya Mexico na ubalozi wa Iran mjini Mexico City zimesema kuwa, ni wazi  kwamba Marekani imefanya kosa hilo kubwa la kistratijia na ndio maana inafanya juhudi kubwa za kuhadaa na kuzipotosha nchi za Amerika ya Latin ili zinyamaze kimya na kutolaani hatua hiyo ya kigaidi.

Gazeti la Kimarekani la Wall Street Journal linaloeneza uongo dhidi ya Iran

Idara ya mahusiano ya umma katika Wizara ya Mambo ya Nje ya Mexico sambamba na kutuma jibu kwenda kwa gazeti hilo la Kimarekani imesema, kile kilichoandikwa katika gazeti hilo kuhusiana na ukuruba wa serikali ya Mexico na Iran hasa baada ya kuingia serikali mpya nchini humo, hakina ukweli wowote. Aidha ubalozi wa Iran nao umejibu tuhuma za gazeti la Wall Street Journal kupitia gazeti la El Economista la Mexico.

Tags

Maoni