Jan 19, 2020 02:58 UTC
  • Pentagon yatoa madai ya kuchekesha kuhusiana na hasara iliyoipata katika shambulio la Iran

Kufuatia kufichuliwa baadhi ya hasara zilizotokana na shambulio la makombora ya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran katika kambi ya kijeshi ya Marekani ya Ain Assad, Wizara ya Ulinzi ya Marekani (Pentagon) inafanya njama za kuhalalisha ufichaji hasara na uharibifu wa shambulio hilo, kwa kudai kwamba ilichelewa kufahamu suala hilo.

Kuhusiana na jambo hilo Jonathan Hoffman, Msemaji wa Wizara ya Ulinzi ya Marekani amedai kwamba wizara hiyo ilitambua habari ya kujeruhiwa askari wake baada ya wiki moja kupita tangu kujiri shambulizi hilo la Iran kwenye kambi hiyo ya Marekani nchini Iraq. Sambamba na kukadhibisha kwamba anakusudia kuficha habari inayohusiana na hasara na uharibifu wa shambulio hilo la makombora ya Iran kwenye kambi mbili za kijeshi za Marekani nchini Iraq, Hoffman amedai kuwa makamanda wa kijeshi mjini Washington walifahamu siku ya Alkhamisi iliyopita habari ya kuhamishwa askari 11 wa Marekani kwenda nje ya Iraq kwa ajili ya matibabu kufuatia shambulizi hilo na kwamba ni masaa machache baadaye ndipo Mark Esper, Waziri wa Ulinzi wa nchi hiyo akatangaza rasmi habari hiyo.

Sehemu ndogo ya uharibifu mkubwa uliofanywa na makombora ya Iran kwenye kambi za kijeshi za Marekani nchini Iraq

Itakumbukwa kwamba tarehe 8 mwezi huu Jeshi la Walinzi wa Mapindizu ya Kiislamu ya Iran IRGC lilitoa jibu kali ikiwa ni katika kujibu jinai za jeshi la Marekani baada ya kumuua kigaidi Luteni Jenerali Qassem Soleimani, Kamanda wa Kikosi cha Quds cha jeshi hilo la Iran. Katika jibu hilo IRGC ilishambulia kwa makombora kambi ya kijeshi ya Ain Assad ya Marekani katika mkoa wa Al-Anbar na kambi nyingine ya kijeshi ya nchi hiyo vamizi katika mkoa wa Erbil nchini Iraq. Baadhi ya duru za habari zimeeleza kwamba askari wengi wa Marekani waliangamizwa na kujeruhiwa katika shambulizi hilo la ulipizaji kisasi, kiasi kwamba hakukuwepo na uwezekano wa kuwatibu katika eneo hilo na hivyo wakawa wamepelekwa kwa helikopta katika hospitali ya Marekani mjini Baghdad. 

Maoni