Feb 15, 2020 14:24 UTC
  • Rais wa Ufaransa amjibu waziri wa mambo ya nje wa Marekani akisema: Magharibi 'inadhoofika'

Rais Emmanuel Macron wa Ufaransa amejibu madai ya Waziri wa Mambo ya Nje wa Marekani aliyotoa katika Mkutano wa Usalama wa Munich kwa kusema: Magharibi inadhoofika na kuporomoka.

Akihutubia mkutano huo wa usalama unaofanyika mjini Munich, Ujerumani leo, Macron ameashiria madai ya waziri wa mambo ya nje wa Marekani Mike Pompeo aliyedai kuwa mustakabali wa Magharibi na Shirika la Kijeshi la NATO ni wenye kung'aa na akasema: Tangu miaka michache nyuma Marekani imekuwa ikitekeleza sera ambazo hazihusiani na serikali ya sasa pekee ambazo zina muelekeo wa kujiondoa na kuangalia upya uhusiano wake na Ulaya.

Rais wa Ufaransa ameeleza kusikitishwa na mwenendo unaoelekea kuidhoofisha Magharibi na akasema: Ulaya sasa inabadilika kuwa bara ambalo halina imani tena juu ya mustakabali.

Pompeo akihutubia Mkutano wa Usalama wa Munich

Karibu miezi miwili iliyopita pia sambamba na kukaribia kufanyika kikao cha viongozi wa nchi wanachama wa Shirika la Kijeshi la NATO, Rais wa Ufaransa alitoa hotuba iliyoibua malalamiko aliposema: Shirika hilo la kijeshi limekufa ubongo.

Wakati Pompeo alipohutubia mkutano wa usalama unaofanyika Munich, Ujerumani, mbali na kukosoa hotuba hiyo ya Macron kuhusu NATO alidai pia kwamba Magharibi na NATO zinapiga hatua pamoja kuelekea ushindi.../

 

Tags

Maoni